Ni Ijumaa nyingine tena ambapo
Mapaparazi Wetu, Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’, Musa Mateja ‘Tozi’,
Richard Bukos ‘Mpiga Picha Mkuu’, Shani Ramadhani ‘Mama Libeneke’ na
Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ walijiachia katika viwanja mbalimbali
kusaka matukio na kuwasiliana moja kwa moja na Mkuu wao aliyekuwa Makao
Makuu ya ofisi za gazeti hili zilizopo Bamaga, Mwenge jijni Dar es
Salaam.
Mkuu anacheki saa yake ambayo inamuonesha kuwa ni muda muafaka wa
kupokea matukio kutoka kwa waandishi wake na moja kwa moja anaanza
kumpigia simu Shani Ramadhani ‘Mama Libeneke’.
Saa 4:17 usiku
Saa 4:17 usiku
MASHABIKI WAWEKEANA DAU KWA DIAMOND NA ALI KIBA
Makao Makuu: Shani Ramadhani ‘Mama Libeneke’ pande zipi? Nipe ripoti.
Shani: Mkuu nipo maeneo ya Rose Garden hapa, nilikuwa naelekea Mikocheni nikasikia watu wanabishana kuhusiana na shoo ya Tigo Kiboko Yao ambayo itawakutanisha mafahari wawili ambao hawaishi katika zizi moja, Ali Kiba na Diamond.

Makao Makuu: Hee hawa Tigo wanataka kuzua balaa kwa mashabiki, sasa imekuwaje?
Shani: Kuna wengine ni Timu Diamond na wengine ni Timu Ali Kiba sasa wanabishana eti nani atakuwa kiboko ya mwenzie, inaonekana watu wamekaa mkao wa kula
kusubiri nani ataibuka kidedea.

Makao Makuu: Dah hiyo sasa kali, hakikisha hutoki hapo mpaka ujue mwisho wao utakuwaje.
Shani: Naona sasa wameafikiana wanasema eti kama akishinda Diamond, Timu Ali Kiba itawalipa timu Diamond na ikitokea hivyo kwa Ali Kiba basi Timu Diamond watawajibika.
Makao Makuu: Dah! Basi kuna watu watafaidika sana kupitia hii shoo, kwani wamewekeana dau la shilingi ngapi?

Shani: Wamesema kila mtu atatoa elfu hamsini
Makao Makuu: Sawasawa endelea kupiga kazi ngoja nimpigie Musa Mateja.

Saa 5:10 usiku
MREMBO AZIMIKA, AMGANDA CHAZ BABA
Makao Makuu: Mateja umefichwa wapi muda wote nakupigia simu hupatikani?
Mateja: Mkuu sijafichwa wala nini sema nilikuwa mtaani kwangu naangalia gemu ya Man U na Kombe la Afcon lakini sasa nipo hapa Cheetoz Lounge ‘Miti Mirefu’ Sayansi, Kijitonyama.
Makao Makuu: Mbona hupatikani hewani unataka kuniambia mpira ndiyo umekufanya uzime hadi simu?
Mateja: Hapana mkuu itakuwa tatizo la mtandao tu.

Makao Makuu: Haya niambie ulichokiona hapo hadi muda huu.
Mateja: Mkuu hapa kuna dansi la kufa mtu linaporomoshwa na Bendi ya Mashujaa lakini kitu cha ajabu kuna mdada hapa kalewa anakata mauno balaa.

Makao Makuu: Eeeh hizo ndiyo habari ninazozitaka alikuwa anakunywa chibuku nini au kaanzia viroba?
Mateja: Kwa ninavyomuona huyu siyo bia tu lazima kaanza na viroba hapa kaja kukazia na bia mbili ila anakoelekea utasikia anachezea viganja vya mke wa Chaz Baba maana anajifanya kalewa sasa kila akicheza anaonekana kumganda sana Chaz Baba.

Makao Makuu: Kweli huyo atakuwa kaanza na viroba, anamfanya nini Chaz Baba?
Mateja: Naona kila akiingia kucheza haishi kumkumbatia na zaidi Chaz anapomaliza kuimba sehemu yake lazima huyu mrembo naye aache kucheza na kumwangalia anapoenda kukaa sijui anataka kujimilikisha?
Makao Makuu: Hiyo imekaa poa kama vipi dili naye mpaka mwisho ili tupate cha kuanzia kesho.
Mateja: Usijali mkuu nipo hapa kuhakikisha nafanya kila liwezekanalo ili kesho tuungurume vizuri.
Makao Makuu: Basi nikutakie usiku mwema kijana wangu.
Mateja: Ahsante, nawe pia Mkuu.

Saa 6:12 usiku
CHANGUDOA AMUINGIZA MJINI MWANAMUZIKI WA B-BAND
Makao Makuu: Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’ upo pande zipi?
Mnally: Kiongozi leo nipo na Bukos ndani ya Club East 24 hapa Mikocheni.
Makao Makuu: Duuh! Kuna nini hapo leo?

Mnally: Mkuu kama kawa hapa leo kuna onesho la B- Band chini ya mkali
Banana Zorro lakini sasa ameshuka jukwaani kidogo namuona anahojiwa na
Bukos juu ya skendo ya kuwa na nyumba ndogo maeneo ya Yombo Buza.
Makao Makuu: Ahaa mwambie amhoji vizuri tupate data kamili kabla ya kumlipua. Vipi upande wako kuna chochote ulichonasa?
Mnally: Ndio Mkuu, kuna huyu mwanamuziki wa Banana, Siz Q ameingizwa mjini na changudoa.
Makao Makuu: Heee! Ilikuwaje?

Mmally: Alinunua bia na kuiweka lakini wakati anataka kuanza kunywa
akaitwa jukwaani kuimba, changu mmoja akaipitia bia hiyo na kuondoka
nayo.
Makao Makuu: Hahaaa! Enhe nini kilichoendelea?
Mnally: Kumbe mshikaji wakati akiwa jukwaani alimuona yule changu akiondoka na bia aliposhuka tu akamfuata na kumlamba kibao kisha kumwaga bia hiyo.

Makao Makuu: Duuh! Hiyo kali ya mwaka endelea na kazi Mnally ngoja nimcheki Shekidele.
Mnally: Ok.
Mnally: Ok.
Saa 7:26 usiku
WACHINA WANASWA WAKIKATA MAUNO UKUMBINI
Makao Makuu: Kijana huu ni muda wa kazi nipe ripoti haraka uko pande zipi?
Shekidele: Mkuu nipo katika Ukumbi wa Samaki Sport, Bendi ya Bikon Sound inafanya makamuzi hapa.
Makao Makuu: Kuna tukio gani ambalo umelinasa mpaka sasa?

Shekidele: Mkuu hapa kuna mashabiki wa Yanga wengi sana wamevalia
nguo zenye rangi ya njano na kijani kutoka Dar kama unavyojua wamekuja
kuangalia mechi kati ya Yanga na Polisi Moro.
Makao Makuu: Sasa ukumbi wote si utakuwa umetawaliwa na Yanga tu?

Shekidele: Acha tu Mkuu sijui hawana hata pesa ya kukodisha vyumba
vya kulala maana kuna wengine hapa uzalendo umewashinda wanasinzia
kwenye meza, lakini nimenasa tukio jingine.
Makao Makuu: Safi sana Mkude Simba ni tukio gani hilo?
Shekidele: Kuna wakandarasi wawili wa Kichina nawaona hapa wanakata mauno balaa sasa hawa dada zetu wanaofanya kazi za usiku tayari wameshawateka.

Makao Makuu: Loh! Hao nao hata huwa hawachelewi, sasa imekuwaje?
Shekidele: Muda huu wamekaa meza moja watu wanacheka sana kwa sababu hawa wachina hawajui Kiswahili na Waswahili pia hawajui Kichina sasa wanawasiliana kwa ishara kama mabubu.
Makao Makuu: Dah! Balaa hilo sasa tatizo nao wamezidi kuparamia watu, wapigie wenzio waambie mkapumzike. Halafu Mayasa Mariwata ‘Kipotabo’ alikuwa hapokei simu yangu mwambie ajiandae kukatatwa ‘alawansi’ yake.

Shekidele: Sawa Mkuu.

إرسال تعليق