Polisi nchini Ujerumani wanasema kuwa kumekuwa na shambuli la kuchoma moto
ofisi za gazeti ambalo lilichapisha vibonzo kutoka kwa gazeti la vibonzo la
Charlie Hebdo.

Mawe na vitu vinavyowaka moto vilirushwa katika dirisha la ofisi za gazeti
la Hambuger Morgenpost mapema leo Jumapili.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Vyumba viwili kwenye afisi hizo viliharibiwa lakini moto huo ulizimwa kwa haraka na hakuna mtu aliyejeruwa. Wiki iliyopita gazeti hilo lilichapisha picha za vibonzo vya mtume Mohammed kutoka gazeti la ufaransa la Charlie Hebdo.

Makala kwenye tovuti ya gazeti hilo inasema haijabainika iwapo shambulizi
hilo lina uhusiano na kuchapishwa kwa picha hizo.
Polisi mjni Hamburg wanasema kuwa wamewakamata vijana kufuatia kisa hicho.
Picha na Yahoo, Habari na BBc Swahili


إرسال تعليق