HAFLA YA KUAPISHWA KWA RAIS WA MSUMBIJI FILIPE JACINTO NYUSI

Rais Mpya wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akila kiapo cha urais
kuiongoza nchi ya Msumbiji jijini Maputo Msumbiji
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye aliwasili Maputo, mji mkuu wa Msumbiji, usiku wa Jumatano, Januari 14, 2015, jana alihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa nchi hiyo, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi.   
Sherehe hizo zilifanyika Independence Square, mjini Maputo jana, Alhamisi, Januari 15, 2015. Mheshimiwa Nyusi anakuwa Rais wa nne wa Msumbiji tokea uhuru wa nchi hiyo mwaka 1975.

 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zambia
Kenneth Kaunda wakati wa kuapishwa kwa Rais mpya wa Msumbiji Felipe Jacinto
Nyusi jijini Maputo Msumbiji jana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mfalme Letsie III  wa
Lesotho(Kushoto), Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia(wapili kushoto) na
kulia ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Viongozi hao walihudhuria sherehe
za kuapishwa kwa Rais Mpya wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi zilizofanyika
jijini Maputo Msumbiji jana

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais Mpya wa Msumbiji Filipe
Jacinto Nyusi muda mfupi baada ya kuapishwa jijini Maputo Msumbiji

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais Mpya wa Msumbiji
Filipe Jacinto Nyusi pamoja na Rais wa Msumbiji aliyemaliza muda wake
Armando Emilio Guebuza katika viwanja vya ikulu ya  Maputo leo baada ya
sherehe za kuapisha leojana.(picha na Freddy Maro)

Kiongozi mwingine mkuu wa Tanzania aliyealikwa kuhudhuria sherehe hizo ni Rais wa Tatu wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, ambaye alifuatana  na mkewe, Mama Anna Mkapa.
Ujumbe wa Tanzania kwenye sherehe hizo ni pamoja na Mama Salma Kikwete, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mahadhi J. Maalim,  Mheshimiwa Mohamed Abood Mohamed ambaye ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Philip Mangula ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM,  Mheshimiwa John Magale Shibuda ambaye ni Mbunge wa CHADEMA na Mheshimiwa Halima Dendegu ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Post a Comment

Previous Post Next Post