Rais Mpya wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akila kiapo cha urais
kuiongoza nchi ya Msumbiji
jijini Maputo Msumbiji |
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye aliwasili
Maputo, mji mkuu wa Msumbiji, usiku wa Jumatano, Januari 14, 2015, jana alihudhuria
sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa nchi hiyo, Mheshimiwa Filipe Jacinto
Nyusi.
Sherehe hizo
zilifanyika Independence Square, mjini Maputo jana, Alhamisi, Januari 15, 2015.
Mheshimiwa Nyusi anakuwa Rais wa nne wa Msumbiji tokea uhuru wa nchi hiyo mwaka
1975.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zambia
Kenneth Kaunda wakati wa
kuapishwa kwa Rais mpya wa Msumbiji Felipe Jacinto
Nyusi
jijini Maputo Msumbiji jana |
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais Mpya wa Msumbiji Filipe
Jacinto Nyusi muda mfupi
baada ya kuapishwa jijini Maputo Msumbiji |
Kiongozi
mwingine mkuu wa Tanzania aliyealikwa kuhudhuria sherehe hizo ni Rais wa Tatu
wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, ambaye alifuatana na mkewe, Mama Anna Mkapa.
Ujumbe wa
Tanzania kwenye sherehe hizo ni pamoja na Mama Salma Kikwete, Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje Mheshimiwa Mahadhi J. Maalim, Mheshimiwa Mohamed Abood Mohamed ambaye
ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Philip Mangula ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa
CCM, Mheshimiwa John Magale Shibuda
ambaye ni Mbunge wa CHADEMA na Mheshimiwa Halima Dendegu ambaye ni Mkuu wa Mkoa
wa Mtwara.
إرسال تعليق