Tukila vyakula vya wanga kama vile wali, ugali, mikate, ndizi,
mihogo, viazi, chapati, vitumbua na maandazi mwili hupata sukari ambayo
bila ya kuwapo mtu atakufa.
Ili mtu aweze kufikiri vizuri, kupumua, kulima,
kubeba mizigo, kutembea, kusoma, kutazama, kusikiliza, dawa alizokunywa
kufanya kazi, lazima mwili wake upate nishati ya kutosha kutoka katika
vyakula anavyokula.
Vilevile, nishati inahitajika kwa mjamzito au mtoto aliyezaliwa ili aweze kukua vizuri.
Vyakula vya mafuta na sukari kama soda, keki na
asali, ingawa navyo vinaupa mwili nishati, vitumike kwa kiasi kidogo ili
kuepusha maradhi mbalimbali.
Mtu kuwa na kiwango kinachotakiwa cha sukari
mwilini ni muhimu sana ili kudhibiti uzito na unene kupita kiasi na
magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya
moyo na saratani. Kama mtu kiwango chake cha sukari kinapanda mara kwa
mara, yupo katika hatari ya kupata magonjwa mengi na hivyo kuwa katika
hatari ya kufa.
Mtu mwenye kiwango cha kupanda sukari cha kudumu
anashauriwa akamwone daktari wake au mtaalamu wa vyakula ampe nasaha za
jumla kuhusu ulaji unaomfaa. Zaidi ya hayo, mtu huyo atashauriwa namna
ya kubadili mtindo wake wa maisha kama vile kufanya mazoezi bila ya
kukoma, kuacha kuvuta sigara na kuacha kunywa pombe.
Lazima tujenge tabia ya kwenda hospitali kupima afya zetu ikiwamo kupima urefu, uzito, wingi wa sukari na mafuta mwilini.
Kupunguza ulaji kwa wingi wa vyakula vya wanga na
mafuta, kunaweza kusaidia kushusha kiwango cha sukari mwilini, hasa kwa
watu wasiofanya mazoezi au kazi za kutoka jasho.
Ulaji unaofaa wa vyakula vya wanga pia, unaweza
kulikabili tatizo la mtu kushuka kiwango cha sukari kuliko inavyotakiwa
kiafya baada ya mtu kula.
Dalili za mtu kupungukiwa sukari katika damu ni
pamoja kuwa na ganzi, kuwa na wasiwasi, kutetemeka, kusikia njaa na
kuchanganyikiwa.
Mtu akinywa vinywaji vyenye kafeini kama vile chai
au kahawa au akiwa na msongo wa mawazo, tatizo lake la kushuka sukari
linakuwa kubwa zaidi.
Moja ya sababu ya kushuka sukari mara baada ya mtu
kula chakula ni mtu kula vyakula vyenye wanga vinavyofyonzwa kwa haraka
tumboni.
- Mwananchi
- Mwananchi
إرسال تعليق