Hali ya mwanamuziki Banza Stone ambaye yuko Tunduma mkoni Mbeya inaendelea vizuri na anatarajiwa kurejea Dar es Salaam Jumatatu mchana kwa shirikia la ndege la Fast Jet.
Kwa
siku mbili zilizopita, hali ya Banza ilikuwa mbaya huku huduma za
kimatibabu zikichelewa, lakini kwa msaada wa wasamaria wema baadae
mwanamuziki huyo akapelekwa hospitali, hali iliyosaidia kuleta ahueni.
Kwasasa Banza yuko uraiani (kasha toka hospitali) na yupo tayari kwa safari ya kurejea Dar es Salaam.
Taarifa
kutoka kwa mdau Deo Mutta ambaye amekuwa akifanya mawasiliano ya mara
kwa mara na watu wa Tunduma inasema hivi (inawekwa kama ilivyo bila
kupunguza wala kuogeza neon): Ninaomba kutoa taarifa ya hali ya Mgonjwa
wetu Ramadhani Masanja Banza Stone Mwalimu wa Walimu. Nimeongea na Banza
asubuhi hii anaendelea vyema na yuko Tayari kwa Safari. Mgonjwa
ataondoka Mbeya Kesho kwa Fast Jet na kufika Dar es salaam saa nane
mchana. Utaratibu wa airport uko kama ifuatavyo. Bwana Hamis Magodoro na
Hamis Masanja (Kaka yake Banza watampokea Airport na kumpeleka Nyumbani
Sinza na Baadaye Atakwenda kwenye Clinic yake Sinza Palestina. Jana
Band ya Utalii Band ilituma shilingi 51,000/= Kwangu kupitia kwa Wadau
wawili wa Muziki Jimmy Kamuzora na Benn Kaguo. Pesa hiyo nimempatia
Hamsi Magodoro kwa ajili ya KUKODI TAXI kwenda Airport kumchukua
Mgonjwa. Ninaomba kuweka mazungumzo yangu ya moja kwa moja kati yangu na
Rahim na pamoja na maongezi yangu na Hamis Magodoro. Mazungumzo yangu
na Banza Sitayaweka hapa kwa kuwa asilimia kubwa amezungumzia mambo yake
BINAFSI KIAFYA ... hivyo Siyo uungwana kuyaweka IN PUBLIC. Naomba
kiwasilisha.
Post a Comment