Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,CP Suleiman Kova
--

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa
kukamata silaha moja aina ya SMG yenye namba BA172288 na risasi kumi na
tatu wakati wa mapambano makali ya ana kwa ana kati ya majambazi na Jeshi
la Polisi. Aidha katika tukio hilo majambazi wawili waliuawa kwa
risasi wak ati wakijaribu kuwadhuru askari.
Tukio hilo lilitokea eneo la Kariakoo mtaa wa Mkunguni na
Livingstone saa 3.00hrs usiku. Wakati wa tukio hilo umeme ulikuwa hakuna na
mlalamikaji alikuwa anatumia taa za kawaida. Mara baada ya kuanza tukio
hilo la uporaji wasamaria wema walijulisha Jeshi la Polisi ndipo kikosi maalum
cha kupambana na majambazi (ant robbery squared) kilipofika kwa haraka katika
eneo la tukio tayari kwa mapambano.
Majambazi hao walistuka na kuanza kuwarushia risasi askari
waliokuwa katika gari la Polisi na ndipo sasa kukawa na mapambano ya moja kwa
moja kati ya pande hizo mbili kwa kutumia silaha na kurushiana risasi. Hatimaye
majambazi wawili waliuawa mmoja anayejulikana kwa jina la ALLAN S/O OCHENG @
ONYANGO, Miaka 24, raia wa Kenya aliyepatikana na Pass ya kusafiria yenye
nambari A1688495 iliyotolewa katika mji wa KISUMU nchini Kenya. Jambazi
mwingine aliyeuawa ametambuliwa kwa jina la YUSSUPH S/O HAMIS @ TWALIB, Miaka
46, Mshiraz, Mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Majambazi wengine waliotoroka baada ya tukio hilo wanaendelea
kutafutwa na tunaomba raia wema waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi ili
wapatikane.
Pamoja na kuuawa kwa majambazi hawa na kukamatwa kwa silaha, pia
zimekamatwa pikipiki mbili moja ni SUNLG yenye namba za usajili T249 CMC, rangi
nyekundu. Nyingine ni aina ya BOXER yenye namba za usajili MC350 AM rangi
nyeusi ambazo zote zilitumiwa na majambazi hao katika tukio. Aidha, Jambazi ALLAN
S/O OCHENG @ ONYANGO aliyeuawa amekutwa na simu ya mkononi aina ya TECNO.
MAJAMBAZI WENGINE TISA SUGU WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM
Katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam dhidi ya
ujambazi wa kutumia silaha Jeshi la Polisi limekamata majambazi tisa
wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ya unyang’anyi wa kutumia silaha na makosa
ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.
Oparesheni kali bado inaendelea jijini Dar es Salaam ili
kuhakikisha kwamba majambazi wote wanaotumia silaha pamoja na makosa mengine
ambayo ni kero katika jamii yanashughulikiwa kikamilifu. Pamoja na mafanikio
hayo tunawashukuru raia wema kutokana na juhudi zao za kutoa taarifa mapema
zenye kuwa na mafanikio ya kulifanya jiji la Dar es Salaam liendelee kuwa
shwari.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Post a Comment