Ule msemo wa Kuwa Siku za Mwizi ni Arobaini huenda ukathibitishwa na moja ya kifaa kiitwacho Semenspy kwa wababa au wamama na wanaopenda kwenda kinyume na ndoa zao na wabakaji.
Kifaa hiki kilichobuniwa na kupewa jina la Semenspy kina uwezo wa kubaini majimaji yaliyosalia katika chupi,nguo za kulalia,katika nguo na maeneo mengine baada ya mtu kuhusika katika tendo la ngono.
Vilevile Kifaa hiki kina mwongozo ambao unaofanya mambo kuwa rahisi kwa wanandoa walio na shauku miongoni mwao.
Moja
ya Maagizo yake katika kukitumia ni kwamba pale unapomshuku mumeo ama
mkeo basi unachotakiwa kufanya ni kutafuta majimaji katika chupi au nguo
zilizotajwa hapo awali.
Kifaa hiki cha Semenspy kina weza pia kugundua kuwa endapo mwanamke mjamzito ana uhusiano nje ya ndoa.
Daktari Wachira amesema kuwa kifaa hiki imetengenezwa nchini Marekani na ameweza kubaini kwa kupata majibu sahihi kutoka kwa wanawake wanaotaka kujua iwapo waume zao na marafiki zao wa kiume wanawadanganya katika uhusiano.
Si rahisi kuwakamata wapenzi wanaodanganya kwa kuwa kunahitaji upelelezi zaidi na subra.
kwa kuwa kuna maji maji ya mbegu za kiume katika chupi ya mwanamume sio ushahidi kwamba mwanamume huyo anakwenda nje ya ndoa.
Swali
ni vile utakavyoonyesha ushahidi kwamba maji maji hayo yanatoka kwa
mwanamume huyo kwa kuwa mara nyingi wengi hutoa maji hayo bila ya
kuhusika katika tendo la ngono.
Daktari
Wachira ana shauri kwamba mwanamke anayemchunguza mumewe anafaa kukaa
kwa mda bila kufanya mapenzi, ili kuweza kuchukua sampuli za maji maji
hayo kutoka kwa nguo za mumewe ama mpenziwe.
Anasema kuwa violezi hivyo vinafaa kuchukuliwa mara tatu na kutoka nguo tofauti za mpenzi anayeshukiwa.
Anasema
kwamba si kila mara kwamba maji maji ya mbegu za kiume humtoka
mwanamume bila ya kufanya mapenzi kwa hivyo hhiyo haifai kuwa sababu ya
mwanamume kujilinda.
Swali ni Je endapo kifaa hiki kitaletwa Tanzania unahisi ni nini kitatokea?
إرسال تعليق