HOJA YA MWAKA: Kila kizazi kina jukumu lake kwa taifa husika


Ndugu wasomaji wangu leo ninaanza safari mpya tena ndefu hasa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambao kimsingi ni mgumu sana, kwani rais wetu Profesa Jakaya Kikwete anaondoka na ni lazima tuchague rais mwingine.
Ugumu mwingine ambao ndiyo mkubwa ni mgongano wa vizazi katika uchaguzi ujao, kwani uchaguzi ujao utatawaliwa sana na ajenda ya umri ambalo ni kosa, lakini ajenda yenyewe hasa ni mgongano wa vizazi, kwani kwa kawaida taifa lolote duniani linaongozwa na kizazi kila wakati katika maisha ya taifa husika.
Naandika makala haya mara baada ya Krismasi, pia kabla ya kuvuka mwaka mpya najua mada hii italeta mjadala mkali sana na mpana, kwani ilishaanza kujadiliwa kupitia hoja ya umri, lakini mimi nitaijadili kupitia hoja ya kizazi au vizazi yaani generation.
Ukisoma kamusi ya TUKI toleo la tatu generation maana yake kizazi, three generations maana yake vizazi vitatu (Baba na wanawe na mjukuu) maana nyingine ni kipindi cha wastani cha umri wa mtu wa kuoa na kuwa na watoto, rika,  watu waliozaliwa wakati mmoja, wa rika moja.
Katika uhai wa taifa lolote lile duniani ni uamuzi wa taifa lenyewe kuamua kuongozwa na kizazi gani kila wakati, kwani taifa lazima lizijue changamoto zake linazokabiliana nazo kila wakati ili liweze kujua kwamba kutokana na changamoto zinazolikabili taifa ndizo zinasaidia taifa husika kujua na kufanya uamuzi sahihi na wa busara kwamba waongozwe na kizazi gani katika taifa husika katika jamii yao.
Mwanafalsafa na Mwandishi maarufu wa vitabu ndugu Frantz Omar Fanon ambaye alizaliwa mwaka 1925 aliandika kwenye kitabu chake cha the wretched of the earth  kuwa “kila kizazi lazima kigundue utume wake, ni jukumu lake kuutimiza au kuusaliti utume huo”.
Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliwahi kusema “kila kizazi na kitabu chake”.  Viongozi wote hawa wawili wanachosema ni kwamba kila kizazi kina mambo yake na majukumu ya wakati wake ambayo yanaweza kutekelezwa vyema zaidi na uongozi wa wakati wa kizazi husika. 
Kwa mujibu wa Biblia Yoeli 2:28 na Matendo ya mitume 2:17 Wazee wanatakiwa kuota ndoto na vijana wanatakiwa kutabiri na kuona maono. Vijana na wana hao Mungu anawaona kama wanaona mbele zaidi wakati wazee wanaota ndoto kuwakumbusha vijana yalitokea kuelezea uzoefu wao wa nyuma na kuwashauri vijana nini kifanyike.
 Kwa kifupi wazee ni washauri na vijana ndiyo watendaji maana mahali pengine Biblia inawataja vijana kama wenye nguvu kuweza kukimbia kimbia na kukabili changamoto za wakati huku wakisikiliza ushauri wa wazee wao ambao wamekuwepo duniani kwa muda mrefu na wana uzoefu mkubwa zaidi wa mambo.
---Kutoka na maana na taaluma hii ya kizazi au vizazi mpaka sasa Taifa la Tanzania limeongozwa na vizazi viwili kama ambavyo nimefafanua hapa chini. Hivyo kwa maoni yangu napendekeza kuwa sasa Tanzania iko tayari kuongozwa na kizazi kipya nacho ni kizazi cha tatu na cha uhuru kama mtakavyoona maelezo yangu hapa chini.
Kizazi cha kwanza ni kile kizazi ambacho kilileta uhuru na kuendelea baada ya uhuru ambacho ni cha Rais wa Kwanza wa Tanganyika, Julius Nyerere alizaliwa mwaka 1922, alianza kuongoza taifa akiwa na umri wa miaka 39, aliacha uongozi akiwa na umri wa miaka 63 alifariki akiwa na umri wa miaka 77.
Katika kizazi hicho hicho cha kwanza alitoka Rais wa Pili wa Jamhuri Ali Hassan Mwinyi ambaye alizaliwa mwaka 1925, alipata uongozi kama Rais wa nchi akiwa na miaka 60 na alimaliza akiwa na umri wa miaka miaka 70.

Post a Comment

أحدث أقدم