
Kati ya mambo wanayojiuliza wapenzi wa muziki wa kizazi kipya,
ni uwezo alionao katika kubadilisha mitindo mbalimbali ya uiambaji,
ukilinganisha na wasanii wengine wa kike hapa nchini.
Huyu siyo mwingine ni Vee Money ambaye jina lake
halisi ni Vanessa Mdee, aliyeweza kuonyesha staili tatu tofauti za
uimbaji tangu aingie katika tasnia hiyo mwaka 2012.
Wengi walimjua wakati wa kutafuta mwakilishi wa
kutangaza VJ katika televisheni ya MTV Base. Licha ya kwamba alikuwa
akitangaza kwa muda mrefu, wengi waliamini kwamba kipaji chake ni
utangazaji, vivyo hivyo alivyoingia kwenye muziki. Waliamini kwamba ana
uwezo wa kuimba Pop na R&B, lakini kumbe kipaji chake kinaweza
kutosha katika eneo lolote lile analoamua kukaa kwa wakati wowote.
Vee Money anasema kuwa hatakaa aimbe katika staili
moja ya muziki, kwani anaamini kipaji chake kinampeleka katika muziki
wa aina mbalimbali.
“Mimi ni mpenzi wa muziki wa aina nyingi sana, nasikiliza taarabu, hip hop, injili, dansi yaani kote,” anasema na kuongeza:
“Katika malezi yangu nimesikiliza muziki wa aina
tofauti, baba yangu alikuwa anapenda muziki wa jazz na mama yangu
alikuwa anapenda taarab, huku wakubwa zangu walipenda hiphop, kwa hiyo
nimekuwa nasikiliza ladha zote za muziki huo muda wote wa udogo wangu.”
Vee Money anasema hata katika kutengeneza muziki wake hapendi watu wamwite kama mwanamuziki wa R&B.
“Sipendi hata siku moja niitwe mwanamuziki wa
R&B, narudi kufanya muziki wa kawaida na nitarudi sana kwa sababu
ninapenda kuimba nyimbo za mchanganyiko, za kizungu, kiswahili iwe ni
bongo fleva, Pop, Hiphop kokote kule napenda muziki,” anasema.
Akizungumzia kazi aliyofanya na mwanamuziki,
Barnabas ‘Siri’ anasema amejifunza mengi kutoka kwa mwanamuziki huyo
anayeimba na kupiga ala za muziki.
“Barnaba ni msanii mmoja ambaye anauelewa mpana
sana katika hii fani, ni mtu anayetengeneza muziki mzuri hata mwenyewe
anaweka wazi kwamba anafanya kazi nzuri, lakini si ya kuvuma kama
wafanyavyo wasanii wengine, amechangia elimu yangu kimuziki, ananishauri
na kufanya naye wimbo nimejifunza mengi,” anasema Vee Money.
Anasema hata alipokuwa akitengeneza video yake ya Hawajui aliitumia elimu hiyo kuhakikisha anafanya kazi iliyo bora zaidi.
“Nimeshiriki katika kutayarisha, hata hivyo mawazo
mengine niliyapata kwa Barnaba na msanii wa Afrika Kusini alikuja hapa
nchini, namfahamu kwa muda mrefu nikawa kama mwenyeji wake, nikawa
namwambia kwamba nataka kutengeneza video na God Father, akaniambia
kwamba wapo wengi wanaoweza kufanya,” anasema. Anafafanua kwamba
alimshauri afanye video na prodyuza Nick na ndipo siku hiyohiyo
akazungumza na Nick na kumtumia wazo la nini kifanyike kwenye video hiyo
إرسال تعليق