Mchungaji Christopher Mtikila.
MWANDISHI Eric Shigongo/UWAZI
Tangu mjadala wa mabadiliko ya Katiba ulipoanzishwa na kupitishwa bungeni, kumekuwa na matabaka mawili, moja likitaka katiba iliyoandikwa iungwe mkono na wananchi jingine likidai imechakachuliwa hivyo haifai.

Lakini Bunge Maalum la Katiba limeshapitisha katiba hiyo na
kilichobaki sasa ni kampeni ambayo itahusisha pande hizo mbili.Ni jukumu
la Watanzania kuamua baada ya kusikia hoja za pande mbili ambazo
zitaanza kusikika siku chache zijazo.
Ukweli ni kuwa katiba mpya ya nchi ni lazima kwani kama kuna
mabadiliko ya msingi ya kitaifa ni lazima pia katiba ibadilike. Kwa
mfano wakati tunaingia katika mfumo wa vyama vingi na hata Tume ya Jaji
Nyalali ilishauri katiba ibadilishwe, ikapuuzwa. Kunapokuwa na
mabadiliko kama vile kutoka kwenye utawala wa kikoloni kuja kwenye
uhuru, lazima katiba ibadilike.
Hata wakati Afrika Kusini inapata uhuru kutoka serikali ya makaburu, ilikuwa lazima katiba ibadilishwe.
Mfano mwingine ni Rwanda baada ya kipindi chote cha mapambano na mauaji ya kutisha, ilihitajika kuwe na katiba mpya. Tumeona pia Sudan Kusini ambayo sasa imejitenga na Kaskazini ilihitajika katiba mpya.

Hata Kenya, walianza muda mrefu kudai katiba hadi nchi ilipoingia
kwenye machafuko. Kwa hiyo hayo ni mabadiliko ya msingi ambayo
yanalazimisha kuwepo kwa katiba mpya. Hali hiyo ya kuhitaji katiba mpya
ipo hapa kwetu, wananchi wameonyesha kutoridhishwa na mambo mengi
yanayoendelea nchini. Wanataka kuwe na mfumo mpya utakaoendesha nchi.
Kwa mfano, jambo kubwa linalolalamikiwa na kulazimisha kuwepo kwa
Katiba Mpya ni uchaguzi. Hili pia ni suala lililokuwa kwenye ushauri wa
Tume ya Jaji Nyalali, likapuuzwa. Alishauri iundwe tume huru ya
uchaguzi, siyo kama hii ya sasa ambayo inateuliwa na rais ambaye pia ni
mgombea kwenye uchaguzi.
Wananchi pia wanalalamikia kunyimwa haki ya mgombea binafsi, bunge la
katiba limekataa licha ya Mahakama ya Rufaa Tanzania kukubaliana hilo
na mapendekezo ya Tume ya Jaji Warioba waliweka, ikang’olewa .
Mtu kama unataka kugombea ubunge au udiwani, ni lazima upitie kwenye
chama. Sasa kwenye kampeni tutasikia kwa nini imeng’olewa na wanaopenda
hilo akiwemo Mwenyekiti wa Democratic Party, Mchungaji Christopher
Mtikila watasema kwa nini sheria hiyo iwepo.
Sijui kundi walilokataa hilo watawaambia nini wananchi Kumekuwa na
sheria ya gharama za uchaguzi, lakini haitoi mwanya kwa vyama vidogo
kuwa na matumizi makubwa kama vyama vikubwa.
Sheria hiyo haitekelezeki kwa sababu haijulikani inasimamiwa na nani. Ni Msajili wa Vyama vya Siasa au Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)?
Sheria hiyo haitekelezeki kwa sababu haijulikani inasimamiwa na nani. Ni Msajili wa Vyama vya Siasa au Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)?
Hata huyo, Msajili wa Vyama vya Siasa hana ofisi na watendaji nchi nzima, ataisimamiaje?
Kitu kingine ni mfumo mbovu wa sheria hiyo, kwa mfano Takukuru haieleweki ni jinsi gani itavishughulikia na vyama vingine kwa sababu siyo kila chama kinafuata mfumo wa Chama Cha Mapinduzi.
Kitu kingine ni mfumo mbovu wa sheria hiyo, kwa mfano Takukuru haieleweki ni jinsi gani itavishughulikia na vyama vingine kwa sababu siyo kila chama kinafuata mfumo wa Chama Cha Mapinduzi.
Kwa kweli Takukuru hakuna wanalofanya kuhusu sheria hiyo. Wananchi
wanalalamikia pia sheria ya kutopinga matokeo ya urais. Wanasema hii ni
kasoro, kwa nini matokeo ya rais yasipingwe wakati wabunge na madiwani
wanapingwa?
Wanasema hata Marekani wanapochagua rais wao kuna muda maalum
umewekwa na katiba kabla ya kumwapisha, ili kama kuna dukuduku lolote
litolewe. Wanalalamika hapa nyumbani, tume ikishamtangaza mtu, kesho
yake anaapishwa, haraka ya nini?
Lakini nampongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuunda tume iliyokuwa
inashughulikia katiba mpya japokuwa imemaliza vibaya kwa kubezwa na
baadaye kuibuka makundi mawili ambayo yatapita kwetu kutuambia nini
kizuri kipo na nini kibaya kimeondolewa.
Nchi hii ina maskini wengi na kiukweli wananchi wanajua chanzo cha
umasikini wao, wanajua jinsi kulivyo na mfumo mbovu wa uongozi.Wananchi
wanajiuliza kwa nini Tanzania ni maskini baada ya miaka 50 ya uhuru? Kwa
nini umeme unasumbua? Wanasikia jinsi watu wanavyojilipa fedha nyingi
kama vile kwenye sakata la Richmond, EPA, Dowans na Tegeta Escrow.
Wananchi watataka kusikia kwa wapiga debe wa katiba, nini kimo ndani
ya katiba ambacho kitaziba mianya hiyo ya ufujaji wa fedha za umma. Pia
watataka kujua kwa nini mbunge atawale jimbo kwa miaka 40 na kwa nini
isiwe miaka 10 tu kama ilivyobadilishwa kwa rais?
Tutasikia kampeni za pande hizo mbili na zisijidanganye kupindisha
matakwa ya wananchi, kila upande usome alama za nyakati nasi raia tupime
kila litakalosemwa.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
Post a Comment