Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vijibweni Kigamboni, Dar es Salaam, (CCM), Alice Nehemia.
Stori: Imelda Mtema
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vijibweni Kigamboni, Dar es Salaam, (CCM), Alice Nehemia (pichani) ametoa dukuduku lake la moyoni kwa kupinga vikali baadhi ya watu ambao wanasambaza habari kuwa amechakachua kura hivyo kushinda katika kura zilizopigwa hivi karibuni kuwania nafasi hiyo.

Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, Alice
alisema kuwa uchaguzi huo uliendeshwa na kusimamiwa kwa haki na
kuzingatia weledi mkubwa lakini baada ya matokeo naye kuibuka mshindi,
watu wapatao saba waliandamana kwa madai kuwa ushindi wake ni wa
kuchakachua.
“Ukweli ni kwamba uchaguzi ulipita kwa haki na kuzingatia weledi
mkubwa, sasa wanapojitokeza watu wachache kuharibu inaniuma sana kwa
kuwa najua mimi nilianza kujitoa kwa wapiga kura kabla hata sijapata
cheo hiki, kudai kuwa nimechakachua matokeo siyo sahihi” alisema Alice.
Post a Comment