MWENYEKITI:- SIJACHAKACHUA MATOKEO JAMANI

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa  Vijibweni  Kigamboni, Dar es Salaam, (CCM),  Alice Nehemia.
Stori: Imelda Mtema
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa  Vijibweni  Kigamboni, Dar es Salaam, (CCM),  Alice Nehemia (pichani) ametoa dukuduku lake la  moyoni  kwa kupinga vikali baadhi ya watu  ambao wanasambaza habari kuwa amechakachua kura hivyo kushinda katika kura zilizopigwa hivi karibuni kuwania nafasi hiyo.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita,  Alice alisema kuwa  uchaguzi huo uliendeshwa na kusimamiwa kwa haki na kuzingatia weledi mkubwa lakini baada ya matokeo naye kuibuka mshindi, watu wapatao saba waliandamana kwa madai kuwa ushindi wake ni wa kuchakachua.
“Ukweli ni kwamba uchaguzi ulipita kwa haki na kuzingatia weledi mkubwa, sasa wanapojitokeza watu wachache kuharibu inaniuma sana kwa kuwa najua mimi nilianza kujitoa kwa wapiga kura  kabla hata sijapata cheo hiki, kudai kuwa nimechakachua matokeo siyo sahihi” alisema Alice.

Post a Comment

أحدث أقدم