Ni
Jumatatu nyingine nzuri tunapokutana katika uwanja wetu huu,
nakukaribisha kwa moyo mkunjufu ujumuike nami jamvini. Wiki iliyopita,
tulianza kujadili mada yetu kama inavyojieleza kwa kuhoji kwamba kipigo
kinaweza kusaidia kumnyoosha mwenzi wako?
Nianze kwa kukushukuru wewe ambaye ulituma ujumbe wako mfupi wa maandishi (SMS) ukichangia mada hii. Maoni yako ni ya muhimu sana na binafsi nimejifunza kitu kikubwa kutoka kwako.
WENGI WANACHUKIA SANA KUPIGWA
Wanawake wengi waliopo ndani ya ndoa na wale ambao bado hawajaingia kwenye ndoa, inaonesha kwamba hakuna kitu wanachokichukia kama kupigwa na wenzi wao.
Wapo ambao wametoa ushuhuda wa jinsi walivyoamua kukatisha ndoa zao kwa sababu ya vipigo na ubabe wa waume zao. Wengine wameeleza jinsi walivyoamua kuwakimbia wenzi wao bila taarifa, kwa sababu ya kuchoshwa na vipigo na manyanyaso ndani ya ndoa.
Nilichokibaini ni kwamba hakuna mtu anayependa kupigwa, kutukanwa au kunyanyaswa na mwenzi wake kwa sababu tu ya mapenzi. Kama wewe ni mwanaume na unataka kudumu kwenye ndoa yako, acha mara moja tabia ya kumpiga mwenzi wako.
KIPIGO HUONGEZA KIBURI
Kingine nilichokibaini, wanawake wengi hubadilika kitabia na kuwa wajeuri au wenye kiburi, kwa sababu ya kupigwa na wenzi wao.
“Kama nimefanya makosa, ni bora mume wangu anirekebishe kwa upole, mimi ni mtu mzima naelewa. Lakini akijifanya kutumia nguvu kwa kunipiga au kunitukana, kile alichonikataza nitakifanya maradufu,” huo ni ujumbe kutoka kwa msomaji wangu, Mama Zahoro wa Unguja, Zanzibar.
Kingine cha kujifunza hapa, kama wewe mwanaume kuna jambo hulipendi kuhusu mke wako, kama kweli unataka abadilike, usitumie ubabe au ukali kumrekebisha, zungumza naye kwa upole na bila shaka atakuelewa na kubadilika.
KWA WANAOJITAKIA KUPIGWA
Katika msafara wa mamba, kenge pia wapo. Wakati wanawake dunia nzima wakiunganisha nguvu kupinga ukatili dhidi yao, wapo wengine ambao kwa makusudi kabisa wanajitakia kupigwa na waume au wenzi wao.
Wengi inakuwa ni kwa sababu ya malezi waliyolelewa au maisha waliyowahi kupitia kabla ya kuwa na wenzi wao. Wanaume wengi waliotuma meseji kwangu, walionesha kwamba huwa hawapendi kuwapiga wenzi wao lakini wanalazimishwa kufanya hivyo kutokana na matendo ya wenzi wao.
UFANYEJE ILI USIPIGWE NA MUMEO?
Jibu ni jepesi sana, kitu cha kwanza; wanawake wanapaswa kujiepusha kujibizana na waume au wenzi wao inapotokea kuna ugomvi. Badala ya kuanza kupeana mipasho na mumeo utafikiri unasutana na shoga yako, ni vizuri kunyamaza hata kama unaonewa mpaka hasira zenu ziishe kisha ndiyo mjadiliane kwa upole.
Pia epuka kufanya jambo ambalo mwenzi wako ameshakukataza zaidi ya mara moja. Ukishajua mumeo hapendi ukae vibarazani kutwa ukipiga umbeya, ni vizuri kujitahidi kujizuia kwani ukishindwa kufanya hivyo, huenda ukaamsha hasira zake ukasababisha upigwe.
MWANAMKE HUPIGWA KWA UPANDE WA KHANGA
Mwisho ningependa kusisitiza nilichokieleza awali; tabia ya kupigana kwenye mapenzi siyo nzuri kwa watu wanaopendana ambao wana ndoto za kuishi pamoja kwa maisha yao yote. Kama ulikuwa na tabia hiyo, badilika, jifunze kukabiliana na hasira zako na badala ya kumtwanga mkeo kwa mangumi, muadhibu kwa kumfanyia kitu kizuri. Wahenga wanasema mwanamke hapigwi bali kwa upande wa khanga mpya.
Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.

إرسال تعليق