Mpango huo unajulikana kwa jina la Africoder Dojo ukiwa unaendeshwa na atamizi ya Tehama ya Dar es Salaam
Maimuna Kubegeya, Mwananchi
Teknolojia ya habari na mawasiliano inaendelea kukua na kutumika kwa kiasi kikubwa nchini.
Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Tanzania (COSTECH), kama chombo kinachosimamia teknolojia, inasema kuwa ina wajibu mkubwa wa kuhakikisha teknolojia mbalimbali ikiwamo Tehama zinaendelezwa kwa manufaa ya Taifa.
Mojawapo ya mikakati mbalimbali ya tume hiyo inayolenga kukuza Tehama ni pamoja na kutoa elimu ya kompyuta kwa wanafunzi wa shule za msingi.
Jukumu hili limekabidhiwa Atamizi ya Dar es Salaam (DTBi), inayoendesha mafunzoi hayo yanayolenga kuandaa wataalamu wa kompyuta na Tehama kwa jumla kwa siku zijazo.
AfricoderDojo
Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi, Mhandisi George Mulamula anasema kuwa, mpango huo unaohusisha utoaji wa mafunzo ya utengenezaji wa programu za kompyuta unafahamika kwa jina la AfricoderDojo.
Kupitia mafunzo hayo, wanafunzi wanatengeneza programu mbalimbali zikiwamo zile za utengenezaji wa katuni na michezo ya kompyuta.
“Ni mfumo utakaomuwezesha mwanafunzi kuwa mahiri zaidi kwenye masomo ya sayansi, hivyo kurahisisha maendeleo ya sekta hiyo pamoja na teknolojia nchini,” anasema.
“Katika awamu hii ya kwanza tumefanya mafunzo hayo kwa wanafunzi 30 kutoka kwenye shule tofauti tofauti jijini Dar es salaam,’’ alisema.
Alizitaja shule hizo kuwa ni pamoja na shule za msingi Immaculate, Hekima Waldorf, Shree Hindu Mandal, Libermann na Kijitonyama.
Geofrey Magila ni mwalimu wa teknolojia ya kompyuta anayewafundisha watoto walio katika mpango wa AfricoderDojo. Anasema kwa kiasi kikubwa wameweza kutimiza lengo lao.
“Licha ya kuchukua muda mfupi katika mafunzo haya, wanafunzi wamekuwa na uelewa wa hali ya juu. Muda wa mafunzo ulikuwa ni takriban wiki nane. Lakini cha kufurahisha ni kwamba kwa ujumla wao wameweza kufaulu. Kwa sasa wote wanaweza kutengeneza ‘software’ za kompyuta hususan zile za michezo ya kitoto,” anafafanua.
Anasema watoto wanaoshiriki mpango huu wanaweza kutengeneza programu za kompyuta kutoka hatua ya awali kabisa kiutaalamu inayoitwa ‘script’, hadi kufikia mwisho

إرسال تعليق