Kadri
muda ulivyokuwa unasogea ndivyo mashabiki wa Manchester United
waliosafi na timu kwenda London kuikabali QPR ndivyo walivyozidi
kuhamaki na kuonyesha wazi kuwa bado kuna vitu vya kocha Louis van Gaal
havileti hamasa kwao.
Shambulia,
shambulia, shambulia, ndivyo walivyokuwa wakiimba mashabiki hao
wakionyesha kukerwa na namna iliyokuwa ikitumia muda mwingi kuandaa
mashambulizi katika mechi hiyo ya Ligi Kuu.
Kama vile hiyo haitoshi, mashabiki hao wakataka timu icheze 4-4-2 badala ya 3-5-2 unaotumiwa zaidi na Van Gaal.
Kipindi
cha pili, Mata akapumzishwa na kumpisha Marouane Fellaini na baadae
kidogo mshambuliaji kinda James Wilson akaingia kuchukua nafasi ya beki
Jonh Evans na hapo ndipo mambo yalipoanza kuchanganya, United ikaanza
kusukuma mashambulizi ya mfululizo kwenye lango la QPR. Mashabiki
wakapata kitu roho yao inataka.
Kipa
wa QPR, Robert Green akaibuka kuwa nyota wa mchezo baada ya kufuta
michomo mingi ambayo ambayo yangeweza kufanya Unted iangushe karamu ya
magoli.
Dakika
ya 56 Angel Di Maria alimimina krosi tamu iliyomkuta Falcao ndani ya
box akaachia mkwaju mtamu wa kichwa lakini kwa maajabu ya wengi Green
akaokoa.
Lakini
dakika mbili baadae Antonio Valencia akakimbia upande wa kulia na
kumpelekea pande Fellaini ambaye alipata wasaa mzuri wa kuumiliki mpira
na kuachia shuti lilikwenda wavuni licha kipa kuucheza kwa ncha za
vidole
Ukaja wasaa wa Wilson, kunako dakika ya 90 akaifungia United bao la pili kwa juhudi zake binafisi.
Wilson
alichukua mpira na kuihadaa ngome ya QPR kabla ya kuachia mkwaju
uliopanguliwa na Robert Green, mpira ukarudi tena kwa Wlison ambaye
hakufanya ajizi akafunga kwa shuti kali la karibu.
QPR
(4-4-2): Green 8.5; Isla 7, Dunne 6.5 (Caulker 46 - 6), Onouha 6, Hill
6; Vargas 5.5, Henry 6, Barton 5, Fer 6 (Taarabt 70 - 5); Austin 7,
Zamora 7 (Kranjcar 71 - 4)
Manchester
United (3-5-2): De Gea 8; Jones 7.5, Evans 7, Rojo 7; Valencia 7,
Carrick 7.5, Mata 4, Blind 7, Rooney 7.5; Di Maria 7, Falcao 5.
Post a Comment