LICHA YA USHINDI 2-0 MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED WAANZA KUCHOSHWA NA MFUMO WA VAN GAAL


Kadri muda ulivyokuwa unasogea ndivyo mashabiki wa Manchester United waliosafi na timu kwenda London kuikabali QPR ndivyo walivyozidi kuhamaki na kuonyesha wazi kuwa bado kuna vitu vya kocha Louis van Gaal havileti hamasa kwao.
Shambulia, shambulia, shambulia, ndivyo walivyokuwa wakiimba mashabiki hao wakionyesha kukerwa na namna iliyokuwa ikitumia muda mwingi kuandaa mashambulizi katika mechi hiyo ya Ligi Kuu.
Kama vile hiyo haitoshi, mashabiki hao wakataka timu icheze 4-4-2 badala ya 3-5-2 unaotumiwa zaidi na Van Gaal.
Kipindi cha pili, Mata akapumzishwa na kumpisha Marouane Fellaini na baadae kidogo mshambuliaji kinda James Wilson akaingia kuchukua nafasi ya beki Jonh Evans na hapo ndipo mambo yalipoanza kuchanganya, United ikaanza kusukuma mashambulizi ya mfululizo kwenye lango la QPR. Mashabiki wakapata kitu roho yao inataka.
Kipa wa QPR, Robert Green akaibuka kuwa nyota wa mchezo baada ya kufuta michomo mingi ambayo ambayo yangeweza kufanya Unted iangushe karamu ya magoli.
Dakika ya 56 Angel Di Maria alimimina krosi tamu iliyomkuta Falcao ndani ya box akaachia mkwaju mtamu wa kichwa lakini kwa maajabu ya wengi Green akaokoa.
Lakini dakika mbili baadae Antonio Valencia akakimbia upande wa kulia na kumpelekea pande Fellaini ambaye alipata wasaa mzuri wa kuumiliki mpira na kuachia shuti lilikwenda wavuni licha kipa kuucheza kwa ncha za vidole

Ukaja wasaa wa Wilson, kunako dakika ya 90 akaifungia United bao la pili kwa juhudi zake binafisi.
Wilson alichukua mpira na kuihadaa ngome ya QPR kabla ya kuachia mkwaju uliopanguliwa na Robert Green, mpira ukarudi tena kwa Wlison ambaye hakufanya ajizi akafunga kwa shuti kali la karibu.


QPR (4-4-2): Green 8.5; Isla 7, Dunne 6.5 (Caulker 46 - 6), Onouha 6, Hill 6; Vargas 5.5, Henry 6, Barton 5, Fer 6 (Taarabt 70 - 5); Austin 7, Zamora 7 (Kranjcar 71 - 4)
Manchester United (3-5-2): De Gea 8; Jones 7.5, Evans 7, Rojo 7; Valencia 7, Carrick 7.5, Mata 4, Blind 7, Rooney 7.5; Di Maria 7, Falcao 5.

Post a Comment

أحدث أقدم