Imebainika
kwamba, wanaume wanaposaka wapenzi, huwa tayari kutii
masharti wanayopewa na upande wa pili. Utii huu ndiyo
unaotajwa kumvutia mwanawake kiasi cha kumfanya aamini
kirahisi kuwa mwanaume wa maisha yake nihuyo anayemtongoza
wakati huo.Hakuna shaka kwamba, katika mazungumzo ya awali
ya mwanaume anayemteka mwanamke kimahaba, kinywa chake huwa
hakikauki maneno haya manne yenye nguvu ya kumdatisha
mwanamke, ambayo niNAKUPENDA, NAKUHITAJI, SAMAHANI na
ASANTE.
Ni
wazi kwamba kuna wanaume wengi ambao huanza na gia kubwa
ya maneno hao wamebainika kupoteza mvuto wa kimapenzi
waliokuwa nao mwanzo kwa wapenzi wao. Binafsi nathibitisha
hili kwa kuwa nimeshafanya uchunguzi kupitia wanaume
wanaonijia kutaka majibu ya kwa nini wapenzi wao
wamewageuka na kutokuwapenda kama awali.Kabla ya kuwashauri
nimekuwa nawadodosa na hatimaye kutambuakuwa waliacha
kutumia maneno hayo mara tu walipoona wamefanikiwa
walichokuwa wanakitafuta.Kama nilivyosema neno la kwanza
lenye nguvu ya kumteka kimapenzi mwanamke ni
NAKUPENDA.
Neno hili ni tiba inayoponya hofu na kumfanya mwanamke
ajiamini. Neno la pili, NAKUHITAJI. Kama inavyokuwa wakati
wa kutongoza, mwanamke anapenda kuambiwa neno hilo na
kufanyiwa vitendo vinavyoonesha kuhitajika kwake katika
maamuzi, matembezi, faraja na muongozo wa kimaisha. Sambamba
na hilo mwanamke anapenda sana kupewa
ASANTE
katika yale anayofanya. Jambo la mwisho kabisa ni
SAMAHANI. Ndugu zangu kuna wanaume ambao hawako tayari
kuomba msamaha kabisa hata kama wamekosa kosa kubwa na la
wazi kiasi gani? Kifupi tabia hiyo haipendezi. Ni busara
kwa mwanaume kumuomba radhi mpenzi wake, ili naye ajione ni
mwenye mamlaka na hivyo kuzidisha upendo na uangalizi wa
tabia mbaya za mwanaume. Niishie hapa kwa kuwashauri
wanaume kuwa wakitaka kuwateka wanamke kimapenzi watumie
kwa vitendo maneno haya manne
إرسال تعليق