Usiku huu nchini Uswiss ndio mahali ambako macho masikio na mawazo ya
wapenzi wengi wa mchezo wa soka yalikoelekezwa katika ile hafla ya
utoaji tuzo za mwanasoka bora wa dunia maarufu kama Ballon D’or .
Wachezaji watatu wanawania tuzo hii kubwa kuliko zote kwa wanasoka
nao si wengine bali ni Manuel Neur , Lionel Messi na Cristiano Ronaldo
na mmoja wao usiku huu ataweza historia kwa kurudi nyumbani akiwa na
utzo ya nne au ya kwanza kwa wachezaji hawa waliofanya vizuri mwaka
uliopita .
Ronaldo,Neuer na Messi wakiwa kwenye mahojiano na waandishi wa habari mchana wa leo.
Lionel
Messi amekuwemo kwneye tuzo hizi kwa mara nane kabla ya leo na hii
itakuwa mara yake ya tisa kuwepo kwenye orodha ya wachezaji watatu bora.
Cristiano Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya Ballon D’or mwaka huu .
Kombe ambalo mshindi wa tuzo ya Ballon D’or atakabidhiwa usiku huu .
Cristiano Ronaldo akiwa amepozi kwa ajili ya picha mapema hii leo huko Uswissi .
Mmoja kati ya wanaowania tuzo ya kocha bora Carlo Ancelotti akiwa anajibu maswali ya waandishi wa habari.
Kocha Mjerumani Joachim Loew anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka.
Muargentina Diego Simeone naye atakuwa moja ya makocha watatu wanaowania tuzo ya kocha bora wa mwaka .
Kombe ambalo kocha bora wa mwaka atakabidhiwa kwenye tuzo za Ballon D’or.
Cristiano Ronaldo wakati akiwa uwanja wa ndege wa Madrid akielekea kukwea pipa kwenda nchini Uswissi mapema hii leo .
Ronaldo akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Madrid.
Ronaldo na familia yake wakati alipowasili nchini Uswisi hii leo .
Manuel Neuer akiwa na Arjen Robben wakati wakiwa nchini Qatar kabla ya kupande ndege kwenda nchi Uswissi.
Neuer akiwa na Robben wakiwa kwenye ndege ya kukodi njiani kuelekea uswissi.
إرسال تعليق