MUIGIZAJI
mkongwe nchini, Salome Nonge ‘Mama Abdul’ amewacharukia mastaa wa
filamu Bongo kwa kususia kujitokeza katika uzinduzi wa kitabu cha
Kanumba.Muigizaji mkongwe nchini, Salome Nonge ‘Mama Abdul’.
Akizungumza na Uwazi, Mama Abdul aliyasema hayo muda mfupi baada ya
kuisha kwa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki
iliyopita katika Ukumbi wa Landmark, Ubungo Riverside ambapo
alisikitishwa kutokana na marehemu kuwa mchango mkubwa katika tasnia ya
filamu.
“Wasanii wetu ni wanafiki, wanapata wapi
jeuri ya kumtenga Mama Kanumba wakati kwenye msiba walikuwa wote? Au
tuseme wameona kwenye uzinduzi hakuna namna ya kupiga dili kama
walivyozoea watawakosa watu wa kuwauzia sura.”Mama Kanumba( wa tatu kulia) akiwa na wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa kitabu cha Kanumba.
“Wamenikera, halafu wakimuona Mama Kanumba wanajifanya kumsalimia
kinafiki. Bongo hakuna kama Kanumba waache kujishauwa,” alisema Mama
Abdul.
Post a Comment