MSANII
wa kitambo kwenye tasnia ya filamu Bongo, Yvonne Cherly ‘Monalisa’ (33)
amesema kuwa yeye siyo gubegube kwani alishawahi kukaa ndani ya ndoa
lakini sasa ameamua kutulia.
“Mimi si gubegube, nikiamua kurudi na kufunga ndoa naweza tena nitaolewa kama Yvonne Cherly kwani ndilo jina langu halisi. Ninachokiwaza kwa sasa si kukaa ndani ya ndoa bali namna kazi zangu zitakavyoweza kuonekana zaidi,” alisema Monalisa.
Msanii wa kitambo kwenye tasnia ya filamu Bongo, Yvonne Cherly ‘Monalisa’.
Akipiga stori mbili-tatu na Uwazi, Monalisa alisema kuwa hata kama
akiamua kurudi upya kwenye ndoa anaweza na kutilia msisitizo kuwa
mwanaume atayemuoa lazima atambue kuwa anayemuoa ni Yvonne Cherly na si
Monalisa kwani jina hilo litakalokuwepo kwenye cheti cha ndoa.“Mimi si gubegube, nikiamua kurudi na kufunga ndoa naweza tena nitaolewa kama Yvonne Cherly kwani ndilo jina langu halisi. Ninachokiwaza kwa sasa si kukaa ndani ya ndoa bali namna kazi zangu zitakavyoweza kuonekana zaidi,” alisema Monalisa.
Post a Comment