Baadhi ya vigogo katika Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na Dk. John Pombe
Magufuli (pichani), wameikimbia wizara hiyo na kwenda sehemu nyingine
kwa kile walichodai ni uongozi wa kibabe na unyanyasaji katika idara ya
usalama barabarani na mazingira.
Waziri ya Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli.
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu wizarani hapo umebaini kuwa
katika idara hiyo inayoongozwa na Julius Chambo kama Kaimu Mkurugenzi
imekimbiwa na vigogo watatu, Juma Kijavara, Omari Kinyange na Samson
Nkundineza ambao wameondoka wizarani hapo ndani ya mwezi mmoja, Desemba
mwaka jana.
Vyanzo vyetu vya habari ndani ya wizara hiyo vinadai kwamba tangu
Chambo ahamishiwe katika idara hiyo akitokea kituo cha mizani Himo
mkoani Kilimanjaro, utendaji wa kazi umekuwa ukisuasua kwa kile
kinachodaiwa kuwa ni uongozi wa kidikteta pia wameona kama amewekwa hapo
kiupendeleo kwa vile mambo ya utawala hajui.
Katika idara hiyo inayoongozwa na Chambo ilikuwa na wahandisi wanne
lakini baada ya kuondoka kwa hao watatu alibakia mmoja na inasemekana
wameletwa wengine kufidia walioondoka.
Kuhama kwa vigogo hao kumewatia hofu wafanyakazi waliobaki na inasemekana kuwa baadhi yao wanataka kuondoka.
Kuhama kwa vigogo hao kumewatia hofu wafanyakazi waliobaki na inasemekana kuwa baadhi yao wanataka kuondoka.
Aidha baadhi ya wafanyakazi wamelalamikia kipindi kirefu alichopewa kukaimu nafasi hiyo.
“Huwezi kukaimu ofisi kwa muda mrefu namna hiyo hapa kuna tatizo,” alisema mhandisi mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini.
“Huwezi kukaimu ofisi kwa muda mrefu namna hiyo hapa kuna tatizo,” alisema mhandisi mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini.
Aliongeza kuwa kama wizara haitafanya mabadiliko stahiki kuna
wahandisi watatu wataondoka hivyo wizara kupoteza wataalamu wazoefu kitu
ambacho kitaleta shida kubwa wizarani hapo.
Gazeti hili lilipomtafuta Chambo ofisini kwake alikiri kuondoka kwa vigogo hao na akadai kuwa ni mmoja tu ndiye aliyemuaga lakini wengine hawakufanya hivyo.
Gazeti hili lilipomtafuta Chambo ofisini kwake alikiri kuondoka kwa vigogo hao na akadai kuwa ni mmoja tu ndiye aliyemuaga lakini wengine hawakufanya hivyo.
“Mimi naamini wameondoka kwenda kutafuta maslahi zaidi, kuhusu madai
mengine mimi siwezi kuzungumzia masuala ya wizara, nendeni kwa katibu
mkuu,” alisema Chambo. Naye katibu mkuu wa wizara hiyo, Musa Lyombe
alipohojiwa alisema wafanyakazi hao wameondoka Desemba mwaka jana lakini
hata yeye ameshangazwa na kuondoka kwao.
“Nafikiri kuna jambo na kuna umuhimu wa kulichunguza suala hili kwa
karibu, wao walikuja kwangu nikijua wanafuata maslahi, kwa nini itokee
katika idara hiyo moja?” alihoji.
Post a Comment