Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka
ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Ronald Phiri amesema mamlaka
hiyo inaweza kufa endapo nchi washirika hawatawekeza mtaji mkubwa ili
kuongeza uzalishaji.
Kauli hiyo inakuja ikiwa ni siku ya tatu tangu
wafanyakazi wa shirika hilo zaidi ya 1,500 kugoma kuendelea na kazi huku
wakitoa siku saba kwa uongozi wa Tazara kushughulikia madai ya
mishahara ya miezi mitano.
Phiri alisema jana kuwa, hatakuwa tayari
kuzungumzia kero yoyote inayotokana na migogoro ya wafanyakazi na badala
yake amezitaka serikali washirika kutoa ufafanuzi wa changamoto
zinazowakabili.
“Nilishatoa mapendekezo yangu muda mrefu, hivyo serikali hizo zinafahamu hatua gani zinazohitajika,” alisema Phiri.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaban Mwinjake alisema kwa sasa hataweza kuzungumza lolote kwa kuwa yuko likizo
Post a Comment