Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imekiandikia
barua chama cha Tanzania Labour (TLP), kukitaka kifanye uchaguzi wa
viongozi na kwamba endapo hakitafanya hivyo baada ya Aprili, mwaka huu
kitafutiwa usajili.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, alisema sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 kifungu cha 9 inavitaka vyama hivyo kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano, lakini chama hicho kimepitisha muda bila kufanya uchaguzi.
Alisema ofisi ya Msajili ilipokea maombi kwa chama hicho mara tatu kikiomba kusogezewa mbele muda wa kufanya uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali.
Sababu ya kwanza ilikuwa ya Mwenyekiti wake, Augustine Mrema, kuwa nje ya nchi kwa matibabu, sababu ya pili ilikuwa kupisha Bunge Maalum la Katiba na nyingine ilikuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Nyahoza alisema sababu zote hizo zilipimwa na kuonekana za msingi ambazo zilikuwa mwaka jana, lakini hivi sasa hawana sababu nyingine ya kuwazuia kutofanya uchaguzi huo.
“Kama sheria ya vyama vya siasa inavyosema, kufanya uchaguzi kwa vyama ni lazima kila baada ya miaka mitano, TLP ilitakiwa iwe imefanya hivyo mwaka jana, lakini kutokana na sababu za msingi tuliwavumilia, mwaka huu hawana sababu nyingine ya kujitetea, na tumeamua kuwaandikia barua kuwataka wafanye uchaguzi huo ifikapo Aprili mwaka huu, kinyume cha hapo chama kitafutwa,” alisema.
Aidha, Msajili amemwandikia barua Mrema kumtaka awasilishe maelezo kwa ofisi hiyo juu ya tuhuma zinazomkabili za kuendesha chama kinyume cha Katiba ya chama.
Uamuzi wa kumtaka Mrema kuwasilisha maelezo hayo umefuatia malalamiko ya baadhi ya wanachama kumshutumu kuendesha chama kinyume cha kanuni na taratibu za chama.

CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق