Mara nyingi tunazungumzia unene uliokithiri kwa watu wazima pekee huku tukidhani tatizo hilo haliwahusu watoto.
Kutokana na hali ya maisha kubadilika na watu
kubadili mienendo ya maisha kwa kula vyakula vya kisasa vingi vikiwa ni
vile vinavyozalishwa viwandani, magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameanza
kubisha hodi hata kwa watoto na vijana.
Magonjwa hayo yasiyoambukiza ni tatizo la mishipa
ya damu na moyo, shinikizo la damu, kisukari, kiharusi na ugonjwa wa
akili wa kusahau.
Nchi kama Tanzania inayoendelea kukua kiuchumi,
nayo imeanza kuonyesha kuwa tusipochukua hatua tunaweza kufikia kiwango
kama Marekani katika miongo ya baadaye.
Takwimu za kitua cha udhibiti wa magonjwa nchini
Marekani, zinaonyesha kati ya watoto watano, mmoja ana uzito uliokithiri
au uzito mkubwa.
Watoto wenye matatizo haya wengi wao ni watu wazima, watoto ni wachache.
Inaonyesha pia watoto bado hawako katika hatari ya kukumbwa na maradhi yanayoambatana na unene ukilinganisha na watu wazima.
Kwa upande mwingine, watoto hawa wanajiweka katika hatari zaidi ya kuongezeka uzito wakati wa balehe na ujana wao.
Jambo hili linaongeza hatari ya kupata maradhi
sugu yasiyoambukiza ikiwamo magonjwa kama ya moyo na kisukari katika
umri wa ukubwani.
Tatizo hili pia linawaweka katika hatari ya kuwa
katika shinikizo la kiakili, huzuni na kutojiamini kutokana na kujihisi
wako tofauti kimaumbile.
Urithi wa chembehai za unene ni moja ya jambo
linalochangia sana mtu kunenepa. Jambo jingine ni kutojishughulisha
kimwili na ulaji vyakula kiholela bila kuzingatia kanuni za afya.
Ingawa ni mara chache sana kwa mtoto kuwa na homoni zinazoweza kuchangia mtoto kuwa na unene uliokithiri.
- Mwananchi
- Mwananchi
إرسال تعليق