Huenda ile dhana kwamba wasanii wanaogopa kuoa kwa sababu
wanahisi watashuka chati, inaweza ikawa na ukweli ndani yake, kwa mujibu
wa msanii nyota wa hiphop nchini, Ney wa Mitego.
Awalinyota wa muziki nchini na barani Afrika,
Diamond Platnumz aliwahi kunukuliwa mwaka jana akisema kuwa hawezi
kumuoa mchumba wake wa zamani, Wema Sepetu, kauli ambayo baadaye
aliikanusha.
Lakini Ney wa Mitego, ambaye kwa sasa ana mtoto wa
kiume aliyempata kwa mchumba wake, Siwema Oktoba mwaka jana, ameamua
kufunguka akieleza bayana kuwa hana mpango wa kuoa kwa sasa mpaka
akamilishe baadhi ya mambo.
“Sijasema kwamba siwezi kuoa, ila kwa sasa siwezi
kulizungumzia suala hilo. Kuna vitu nakamilisha na vikiwa tayari watu
wote watajua,” alisema rapa huyo. “Ni kweli kwamba Siwema ni mchumba
wangu ninayempenda sana na nashkuru amenizalia mtoto ila mipango yetu ni
baadaye.”
Alipoulizwa kuhusu idadi ya watoto alionao na
iwapo ana mpango wa kumhalalisha Siwema au mwanamke mwingine kati ya
watatu aliozaa nao, Ney alisema:
“Nina watoto wengi, ila kifupi nitakwambia kwamba
ninao watatu na kati ya hawa kila mmoja ana mama yake. Sasa siwezi
kulisemea hili moja kwa moja. Maisha ni duara hujui wapi utagota, lakini
niseme tu kwamba nampenda sana Siwema.”
Ney wa Mitego, ambaye anasema anamiliki nyumba
yenye thamani ya Sh180 milioni, alisisitiza kuwa bado hajamaliza baadhi
ya mambo yake katika muziki, hivyo ni vigumu kuingia kwenye majukumu ya
ndoa kwa sasa.
Hata hivyo picha alizozitupia katika mitandao wiki
hii, zinamwonyesha akiwa amevaa pete inayoonekana kuwa ya ndoa, lakini
alipoulizwa alikuwa na jibu jingine.
“Hahaahaaa pete hii naivaa huu mwaka wa sita sasa,
tangu nilipopewa zawadi na rafiki yangu anayeishi nje ya nchi. Hii ni
zawadi na lazima niitunze kwa kuwa kwanza ninaipenda,” alisema.
Anasema mwonekano alionao hivi sasa ndiyo unaofanya vitu vitu vingi ambavyo watu hawakuwahi kuvichunguza, vionekane.
“Mwonekano wangu mpya kwa sasa ndiyo umewafanya
wengi kunichunguza na kuiona hii pete. Ukweli ni kwamba si ya ndoa na
sijaoa bado, ila watambue kwamba mwaka huu nimejipanga kivingine. Kuna
mambo mengi ambayo nitayafanya kupitia muziki,” alisema.
“Miaka ya nyuma nilikuwa mtu ambaye sijachangamka
sana katika fani. Sasa nataka kwenda kisasa na nifanye kazi ya muziki
kivingine kabisa. Nilikuwa hata video zangu nafanya ndani ya nchi
nikitoka nje ni Kenya nimerudi tena ndani, ila mwaka huu nabadilika na
ndiyo maana unaniona suti kali nini, mambo yanabadilika sasa,” anasema
Post a Comment