Niliipenda hii ya Yanga ilichoifanyia Azam FC

Natumai mambo yanakwenda kama yalivyopangwa. Ni wazi kila mmoja anapambana kuhakikisha mwaka 2015 unakuwa katika mstari wake.
Niwakumbushe. Kati ya Februari 13, 14 na 15, 2015, klabu za Tanzania, Yanga na Azam FC zitakuwa katika harakati za kuwania heshima ya ubingwa kwa klabu Afrika.
Hizo zitakuwa mechi za kwanza na marudiano yake yatakuwa wiki mbili baadaye, na mshindi atasonga raundi ya kwanza.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho, Yanga itaanzia nyumbani (kombe la Shirikisho) kucheza na BDF XI ya Botswana wakati Azam FC nayo itaanzia nyumbani dhidi ya El Merreikh ya Sudan Ligi ya Mabingwa.
Katika michezo hiyo, kimsingi, klabu za Tanzania zina nafasi kubwa kwa kuwa zinaanzia nyumbani na kumalizia ugenini.
Ni kawaida kuwa klabu inayoanzia nyumbani inakuwa na nafasi kubwa ya kufanya vizuri na kujihami ugenini.
Hapa nina yangu mawili, kwanza; nafasi za wawakilishi wetu, na Pili; nafasi ya mashabiki.
Klabu za Yanga na Azam FC ndiyo wawakilishi wetu katika michuano hiyo mikubwa kwa klabu Afrika.
Kama nilivyosema wiki iliyopita kuwa ni nafasi ya timu hizo kufanya upelelezi wa wachezaji wa klabu wanazokumbana nazo.
Mpira wa siku hizi lazima kusomana. Huwezi kuingia uwanjani kucheza na timu kichwakichwa, hiyo ni kizamani sana.
Inatakiwa kusoma mfumo wa timu, kusoma aina ya wachezaji iliyo nao, nguvu iko eneo gani, ni wazi itajenga timu kujiamini.
Ni aibu, na hii huwa inawakuta mno wachezaji na viongozi wetu, kuwa timu zinaingia uwanjani na matokeo yake zinafungwa nyumbani na kuanza kujilaumu sababu hakuna kilichofuatiliwa.

Post a Comment

أحدث أقدم