1. KILA
siku usisahau kumsifia kwa kumwambia ni kiasi gani
alivyo mzuri. Kumbuka kila msichana anapenda kusifiwa
hivyo unapomuambia yeye ni mzuri anaona una mthamini
kuliko msichana yeyote awaye.
2.
Wakati wowote ukipata nafasi muandikie barua au msg
kwenye simu mueleze hisia zako kiasi gani unampenda.
Kumbuka wasichana hupenda kusikia zaidi kutoka kwa
wapenzi wao ni kiasi gani wanapendwa. Haitakiwi iwe
tu katika kipindi cha siku ya wapendanao ndio
umuoneshe kuwa unampenda. Muoneshe msichana ni kiasi
gani yeye ni muhimu sana kwako.
3.
Busu la ghafla na kumshika mkono wakati mkitembea
pamoja itamfanya yeye kujisikia raha zaidi. Na wakati
mwingine msuprise kwa kumtembelea mara kwa mara hi
humfanya akuone wewe ni mtu muhimu pale usipokuwa naye
karibu na kumfanya kukuhitaji zaidi ukiwa naye mbali
4.
Tambua mahitaji yake. Uwe msaada kwake kipindi
ambacho mpenzi wako amekasirika kuwa pale kwa ajili
yake na ukimpooza kwa sauti ya upole na mahaba.
Utashangazwa sana na kiasi gani msaada huo umeleta
mabadiliko kwake. Hakikisha unamsaidia katika shida
zake hapa ndipo kuna tatizo kwa wavulana wengi.
Mapenzi si pesa lakini kuna kipindi ambacho pesa
huitajika kulinda penzi lako. Si msichana anapokuomba
pesa ina maana ana nia ya kukuchuna au amekupendea
pesa kuna
5.
Mchukue mpenzi wako out mara nyingine itamfanya
ajisikie furaha sana kwa sababu wasichana hupenda
enjoyment na boyfriend zao. Hii haitamfanya mpenzi
wako tu kuwa na furaha bali itawafanya nyie kwa
pamoja kujuana na kufahamiana zaidi.
6.
Kuwa muwazi kwake usimfiche jambo linalokuhusu.
Msichana hupenda kutoa ushauri kwa mtu ampendaye
hivyo unapokuwa muwazi atajisikia kuthaminiwa nawe na
kukuona umemuamini
7.
Ukijiona upo busy sana usithubutu kuacha japo
kumpigia simu mara mbili kwa siku hata kama
ukishindwa kumpigia wakati upo ofisini darasani au
kwingineko hakikisha unapopata nafasi japo ujumbe
mfupi wa kumwambia unampenda.
8.
Mkumbatie mara kwa mara katika tukio la kumbatizi
kuna jambo kubwa sana hutokea. Si kwake tu hata kwako
mvulana. Hali ya joto lenu huwaweka pamoja kifikra
hata pale msipokuwa pamoja.
9.
Epuka maugomvi na hasira za mara kwa mara ukiwa nae.
Mwanamke hupenda ustaarabu kwa mtu ambaye yupo
serious naye hivyo ukionesha hasira kabla hata
hujamtongoza unaweza ukamkosa msichana hivihivi
wasichana huwaogopa wavulana wenye hasira na wagomvi
kwa sababu hupenda kubembelezwa.
10.
Mdekeze. Msichana anapenda kudeka anaenda kudeka
sana na kubembelezwa sana hivyo mvulana ukidekewa
usikasirike eti huyu msichana kazidi wewe ndio wakati
wako wa kumuonesha msuchana wako unampenda mdekeze
mpaka aone aibu kudeka siku nyingine. Wasichana
wameumbwa kwa jili ya wavulana ndio maana hudeka hii
ndiyo silaha pekee na ya mwisho kumpata msichana hata
kamasi wako ni wa rafiki yako unaweza ukatumia
silaha hii kumpora msichana huyo kwa mwenzio usipojua
kudekeza utaachwa pia
إرسال تعليق