Wafuasi wa Rais mpya, wakimnadi wakati wa uchaguzi.
Rais mpya wa Sri Lanka Maithripala Sirisena anatarajiwa kuapishwa baadaye leo.
Hatua
hiyo inakuja baada ya Rais anayemaliza muda wake, Mahinda Rajapaksa
kukubali kushindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Alhamisi.
Amekubaliana
na ushindi alioupata mpinzani wake katika uchaguzi huo. Kiongoazi huyo
mpya Maithripala Sirisena aliwahi kuwa waziri katika serikali ya nchi
hiyo.
Msemaji wa Rais wa Sri Lanka amesema Bwana Rajapaksa
ameondoka katika makaazi ya Rais na atahakikisha anayakabidhi madaraka
kiutaratibu.
Baada ya kutangazwa kushindwa kwa Rajapaksa fataki
zilipigwa maeneo mengi ya nchi . Aliitisha uchaguzi mapema kwa matumaini
ya kulinda nafasi yake ya kukaa madarakani kwa awamu ya tatu.(BBC)

إرسال تعليق