---
Siku
ya Jumatano tarehe 31 Desemba 2014 Mwenyekiti wa Muda wa Taifa wa
ACT-Tanzania Ndugu Kadawi Lucas Limbu aliitisha mkutano wa waandishi wa
habari. Katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, alitangaza kuwavua
uanachama Katibu Mkuu wa Muda wa ACT Tanzania ndugu Samson Mwigamba
pamoja na wanachama wengine kadhaa. Ndugu Limbu alieleza kwamba maamuzi
aliyoyatangaza yalifanywa na Kikao cha Kamati Kuu ya ACT Tanzania
ambacho alidai kilifanyika tarehe 30 Desemba 2014. Kupitia taarifa hii napenda kufafanua kuwa:
1.
Hakuna Kikao cha Kamati Kuu kilichoketi katika tarehe iliyotajwa na
Ndugu Kadawi Lucas Limbu. Kikao cha Kamati Kuu kimepangwa kufanyika siku
ya Jumatatu tarehe 5 Januari 2015 Jijini Dar es Salaam, kama
kilivyoamuliwa na Kikao cha Sekratariati cha Tarehe 23 Desemba 2014,
ambacho ndicho chenye jukumu la kikatiba la kuandaa ajenda za vikao vya
Kamati Kuu kwa Mujibu wa Katiba ya ACT-Tanzania (Ibara 37 q (iii)
2. Maamuzi yaliyotangazwa na Ndugu Kadawi Limbu ni batili kwa mujibu wa Katiba ya ACT Tanzania na Sheria ya Vyama vya Siasa Tanzania
2. Maamuzi yaliyotangazwa na Ndugu Kadawi Limbu ni batili kwa mujibu wa Katiba ya ACT Tanzania na Sheria ya Vyama vya Siasa Tanzania
3. Ndugu Samson Mwigamba na viongozi wengine wa muda wa ACT-Tanzania waanaendelea na nafasi zao hadi pale uchaguzi utakapofanyika kwa ratiba itakayopangwa na Kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 5 Januari 2015 au itakavyoamuliwa vinginevyo na vikao halali vya chama.
Pamoja na salamu za uzalendo za ACT-Tanzania
Thomas Matatizo (LLB)
Mwanasheria wa ACT-Tanzania.
31 Desemba 2014
AnwaniSimuBarua Pepe
S.L.P. 105043+255 763463740ACTTanzania@yahoo.com
Dar es Salaam, Tanzania+255 715784670
Mwanasheria wa ACT-Tanzania.
31 Desemba 2014
AnwaniSimuBarua Pepe
S.L.P. 105043+255 763463740ACTTanzania@yahoo.com
Dar es Salaam, Tanzania+255 715784670
Post a Comment