Kpah Sherman.
Tambwe.
KATIKA
hali isiyotarajiwa, mashabiki wa Yanga waliokuwa na dukuduku la moyoni,
juzi Alhamisi jioni walimfuata Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Boniface
Mkwasa na kumtaka abadilishe mpangilio ili badala ya kumtumia straika
Mrundi, Amissi Tambwe kuwa straika wa pili, amchezeshe akiwa straika
namba moja na Mliberia, Kpah Sherman, ndiye awe straika namba mbili.
“Samahani
kocha kwanza pole na kazi, tulikuwa na maoni kwamba Tambwe acheze namba
tisa na Sherman acheze 10, maana tuliona katika Kombe la Mapinduzi
mlikuwa mnawabadilisha sasa tumeona Tambwe anamudu sana tisa hapo
tutapata mabao mengi,” alisema mmoja wa mashabiki hao huku akiungwa
mkono na wenzake waliomzunguka Mkwassa kwenye Uwanja wa Boko Vetereni.
Katika
kutoa ufafanuzi, Mkwasa aliwaambia kuwa hivyo ndivyo walivyopanga
kuwachezesha kwa kuwabadilisha ili kuwazoesha wasikariri namba moja.
Jibu hili
lilionekana kutowaridhisha mashabiki hao, lakini walimshukuru kocha
huyo na kisha kumwambia tangu wameanza kukinoa kikosi hicho kimekuwa na
mabadiliko makubwa na kinawapa matumaini ya kufanya vema katika mechi za
Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.
Katika
hatua nyingine, beki wa Yanga ambaye pia ni nahodha, Nadir Haroub
‘Cannavaro’ amemwambia kocha wa Simba, Goran Kapunovic, kuwa kazi si
kuchukua Kombe la Mapinduzi, bali kushinda mechi za Ligi Kuu Bara.
“Tunaamini
Yanga nzuri ingawa tulitolewa katika Kombe la Mapinduzi, mechi zile si
kipimo kwamba timu yake ni nzuri. Huku kwenye ligi ndiyo sehemu ambayo
Simba inatakiwa kuonyesha ubora wake,”alisema Cannavaro.
“Nimeona
watu wanampongeza sana huyu kocha mpya wa Simba hata mimi nampongeza kwa
ubingwa wa Mapinduzi, lakini ili watu wajue ubora wake anatakiwa
ashinde mechi za ligi.”
Chanzo:Mwanaspoti.
Post a Comment