Katika jitihada za kupambana na uingizwaji wa bidhaa
feki na duni, Shirika la Viwango (TBS), linatarajia kuajiri vijana 200
katika vituo vya mpakani pamoja na viwanja vya ndege kwa lengo la
kuongeza nguvu ili kukabiliana na tatizo hilo.
Msemaji wa shirika hilo Rhoida Andusamile, alieleza hayo wakati akihojiwa na kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One Sterio.
Afisa huyo alisema kuna bidhaa feki sokoni kutokana na kuwa na mianya mingi ya uingizaji wake ikiwa ni pamoja na kuzipitisha mipakani mathalani Tunduma kwa upande wa Zambia , Kasumulu upande wa Malawi, Sirari, Namanga vituo vya mipaka ya Kenya na viwanja vya ndege vya Dar es Salaam na Kia Arusha.
“Tuna mpango wa kuajiri vijana 200, kwa lengo la kuongeza nguvu ya udhibiti wa uingizaji wa bidhaa hafifu nchini, hawa watakuwa na ofisi mipakani pamoja na vituo vya uwanja wa ndege,”alifafanua
Rhoida alieleza kuwa bidhaa zisizo na ubora bado zinazagaa madukani tatizo likiwa ni pamoja na watumiaji kutoelewa madharaa yake na hata wale wanaoyajua wanazifurahia kwa kisingizio kuwa zina bei nafuu tofauti na zile zenye ubora unaotakiwa lakini wanasahau gharama za matibabu ni ghali na madhara yake ni makubwa, iwapo ni za vyakula.
Aidha aliiambia Radio One kuwa shirika hilo limebuni mbinu mbadala wakuwa na alama mpya itakayotumika kwa bidhaa zinazotoka nje. Pia zile ambazo hazina ubora wa kimataifa hazitaruhusiwa kuuzwa nchini, mbinu nyingine ni pamoja na kutoa elimu kwa watumiaji hata kwa wale wafanyabiashara wanaoziuza.
Msemaji wa TBS alisema hatua kali zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya wafanyabiashara wa nguo za mitumba ikiwa ni pamoja na wale wanaouza nguo za ndani na kuwashitaki wanauza nguo zilizopigwa marufuku ambazo hazina viwango.
Hivi karibuni shirika hilo lilifungia kiwanda cha kutengeneza juice mkoani Morogoro na kiwanda cha kutengeneza chumvi cha Sea Salt cha mkoani Pwani kwa tuhuma za kutengeneza bidhaa zisizo na viwango vya kitaifa na kimataifa na zisizojali afya za walaji. Mwaka jana 2014 wafanyabiashara 47 walifikishwa mahakamani na kutozwa faini kwa makosa mbalimbali.
Mdhibiti Ubora wa TBS Deusdedith Pascal, alisema kuwa kiwanda hicho hakitaruhusiwa kuendelea na uzalishaji bidhaa hiyo hadi itakaporekebisha kasoro ikiwa ni pamoja na kuongeza madini joto ndani ya chumvi hiyo.

إرسال تعليق