Fernando
Torres anafungua ukurusa mpya katika historia yake baada ya kufunga bao
lake la kwanza ndani Santiago Bernabeu, kitu ambacho hakawahi kufanya
hapo kabla akiwa na timu yoyote ile.
Hiyo
ilikuwa katika mechi kali marudiano ya kombe la Copa del Rey kati ya
Atletico Madrid na Real Madrid iliyokuwa uwanja wa nyumbani ikipambana
kufuta bao 2-0 ilizofungwa na Atletico kwenye mchezo wa kwanza wiki
iliyopita.
Torres
akatupia bao mbili na kuisadia Atletico Madrid kulazimisha sare ya 2-2
na kusonga mbele kwa jumla ya bao 4-2, hii ikimaanisha kuwa Real Madrid
wametema taji la kwanza miongoni mwa mataji manne waliyoshinda mwaka
jana.
Hii
ni awamu ya pili kwa Torres kuichezea Atletico Madrid timu yake ya
tangu utotoni kabla hajaenda Liverpool, Chelsea na AC Milan.
Katika
awamu yake ya kwanza ya kuitumikia Atletico, Torres hakuwahi kuifunga
Real Madrid hata bao moja, jambo lilifanya mashabiki waliofurika
Santiago Bernabeu Alhamisi usiku wamkejeli wakiamini kuwa hana madhara
yoyote kwao.
Lakini
ilimchukua Torres sekunde 49 tu kuwajibu mashabiki hao baada ya
kuifungia Atletico bao la kwanza lililowafanya Real Madrid wawe na mlima
mrefu wa kupanda.
Beki Sergio Ramos akasawazisha
kwa kichwa dakika ya 20, kabla ya Torres ambaye alifunga bao moja tu
katika miezi yake minne aliyoichezea AC Milan, hajaifungia Atletico goli
la pili dakika ya kwanza tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.
Mchezaji
bora wa dunia Cristiano Ronaldo akaifungia Real Madrid bao la pili
dakika ya 54. Safari ya Real Madrid kutetea kombe hilo la Mfalme
ikakomea hapo.
Kwa matokeo hayo, Atletico sasa itakutana na Barcelona katika hatua ya nusu fainali.
Kwa matokeo hayo, Atletico sasa itakutana na Barcelona katika hatua ya nusu fainali.
إرسال تعليق