Utafiti
mpya unasema aina nyingi za ugonjwa wa saratani ni matokeo ya bahati
mbaya, kuliko malezo ya vinasaba, mazingira na mtindo wa maisha.
Watafiti
nchini Marekani walichunguza aina 31 za saratani na kugundua kwamba
theluthi mbili zilisababishwa na mgawanyiko holela wa seli. Kwa
mgawanyiko wa kila seli kuna hatari ya mabadiliko yanayoweza kusababisha
saratani.Wanasayansi hao wanasema kuimarisha mtindo wa maisha na mazingira kunasaidia kudhibiti magonjwa kama ya saratani ya ngozi na saratani ya mapafu.(BBC)
إرسال تعليق