Siku
ya tarehe 11.01.02 wadau wa "Social Media Network Citizens", ambao ni
watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Twitter walifanya awamu ya pili ya
zoezi la kukabidhi madawati 241 kwa shule ya msingi ya Mjimwema iliyopo
kwenye kata ya Mjimwema, Jimbo la Kigamboni.
Katika awamu
ya kwanza, wadau hawa walikabidhi madawati 45. Jumla ya Tsh 30.5
millioni zimechangwa na wadau hawa na zimetumika kutengeneza madawati
286 yaliyotolewa hadi hivi sasa.
Mchango huu wa madawati
umewezesha kutatua tatizo la madawati kwenye shule hii kwa asilimia 80%
na kuwezesha wanafunzi 858 ambao ni asilimia 75% ya wanafunzi wote kukaa
kwenye dawati.
Mgeni Rasmi kwenye makabidhiano haya alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dkt Faustine Ndugulile.
![]() |
| Mgeni Rasmi, Mbunge wa Kigamboni, akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Social Media Network Citizens na walimu. |
Mwisho,
shule hii bado inahitaji madawati 70 ili watoto wote waweze kuwa na
dawati. Vile vile Ofisi za walimu zina upungufu wa samani. Wadau
wameanza raundi ya tatu ya michango kwa ajili ya kumaliza tatizo la
madawati kwenye shule hii.
Wadau wanaotaka kuchangia wanakaribishwa kuwasiliana na waratibu (@AnnieTanzania na @IrineiKiria) kupitia mtandao wa Twitter.
![]() |
| Mtunza fedha wa Social Media Network Citizens Bi Germana Ibreck akiwa na wanafunzi wa shule ya Mjimwema. |
.jpg)
.jpg)

إرسال تعليق