Serikali imesema mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi
huu itawalipa jumla ya Sh. billion 10 walimu na watumishi wengine kama
sehemu ya madai yao ambayo tayari imeshayahakiki.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani, wakati wa kwenye kipindi cha ‘Kumekucha’ kinachorushwa kituo cha na Redio One.
Alisema kwa mwaka 2014 Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na vyama vingine vya wafanyakazi ilifanya vikao vinne kwa lengo la kuhakiki malikimbikizo ya madeni ya wafanyakazi ili walipwe.
Alisema katika vikao vyote viliweka wazi mambo yote na vilihusisha wawakilishi kutoka kila wilaya na halmashauri husika.
Aliongeza mpaka kufikia Machi hadi Aprili, 2015 Serikali itahakikisha malipo yanakamilika kwa kiasi kikubwa na itabaki sehemu ndogo tu watakayoimalizia baada ya kumaliza kuhakiki malimbilizo hayo.
“Niwatoe hofu watumishi kuwa katika mwaka huu wa fedha mpaka kufikia Juni madai yote yatakuwa yamelipwa kwa kiasi kikubwa,” alisema.
Alifafanua kuwa wakati wa kuhakiki waligundua kuna madeni hewa ambayo Serikali imekuwa ikiwalipa wafanyakazi na kusababisha kuchelewa kwa mchakato wa malipo hayo.
Hata hivyo, Kombani alisema wanaendelea na zoezi la kuhakiki malikimbikizo ya mishahara ya Sh. bilioni nane na yatapokamilika watawalipa wafanyakazi fedha hizo

Post a Comment