Walinzi wavunja ofisi waiba fedha, bunduki



POLISI mkoa wa Shinyanga inawasaka walinzi wawili wa Kampuni ya Prosper Security Guard wakituhumiwa kuvunja ofisi ya Jambo Oil Mill and Ginnery Limited kisha kuiba fedha Sh milioni 1.07 na kutoweka na bunduki mbili aina ya Shot gun na risasi saba.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema tukio hilo ni la Januari 9, mwaka huu saa 1 asubuhi katika eneo la mtaa wa Ibadakuli, kata ya Ibadakuli manispaa ya Shinyanga.
 
Alisema siku hiyo Mkurugenzi wa Jambo Ginnery Mohamed Hawadhi (48) aligundua ofisi ya kampuni imevunjwa na kuibwa Sh 1,070,000 zilizokuwa ndani ya kasiki la chuma mali ya kampuni hiyo.
 
Kwa mujibu wa Kamanda, katika tukio hilo walinzi wawili wa Kampuni ya Ulinzi ya Prosper Security Guard katika ofisi hiyo, walitoweka na bunduki mbili aina ya Shot gun zenye namba F 658126 na R 65967 pamoja na risasi saba.
 
Alitaja walinzi hao kuwa ni William Ubogo na Eliamani Simoni ambao wanatafutwa na polisi ili wakikamatwa hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
 
Hata hivyo Kamanda Kamugisha alisema baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa juu ya uhalifu huo lilifanya msako na Januari 10, mwaka huu saa 6 mchana lilipata silaha zote mbili na risasi saba zikiwa zimetelekezwa katika maficho karibu na kiwanda hicho

Post a Comment

أحدث أقدم