Wasafirishaji wa magari ya abiria mkoani tanga wameiomba serikali
kuchukua hatua haraka kudhibiti baadhi ya wasafirishaji kutoka nchi
jirani ya kenya kuingia nchini kisha kubeba abiria bila kulipa kodi kwa
serikali hatua ambayo ni ukiukwaji wa sheria za usafirishaji za
kimataifa.
Wametoa ombi hilo kwa viongozi wa serikali ngazi ngazi ya mkoa wa
tanga,jeshi la polisi na mamlaka ya udhibiti,usafiri wa nchi kavu na
majini (SUMATRA) katika kikao cha pamoja cha kujadili changamoto
zinazowakabili wasafirishaji na kusababisha matukio ya ajali za
barabarani kushindwa kudhibitiwa.
Wameilalamikia halmashauri ya jiji la tanga kwa kuruhusu
wasafirishaji wenye magari yaliyosajiliwa namba za kenya kuegesha mabasi
yao katika baadhi ya hoteli jijini tanga kisha kuwaamuru wasafirishaji
wazawa kwenda katika kituo kikuu kipya cha kange ili wenzao wa waweze
kuchukua nafasi ya kufanya kazi kwa tija katikati ya jiji bila kulipa
kodi kwa serikali.
Akielezea hatua hiyo kaimu mkurugenzi wa barabara wa mamlaka ya
udhibiti,usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) Bwana Leo Ngowi
amepiga marufuku wenye mabasi hayo kukiuka sheria za usafirishaji za
kimataifa na kutishia kuyafutia leseni za usafirishaji wa kuja nchini
endapo wataendelea kukiuka sheria na taratibu zilizowekwa.

إرسال تعليق