Zaidi
ya watu millioni moja katika mtandao wa facebook wameiona video katika
mtandao kuhusu ajuza moja kutoka Syria anayewakashifu wapiganaji wawili
wa kiislamu akiwaambia ''rudini kwa mungu'' .
Mwanamke huyo aliwakaripia wanaume wawili ambao walikuwa wakichukua kanda hiyo ya video.
''Musiwachinje wenzenu nao pia hawafai kuwachinja''...ni haram...kati yenu na rais Bashar al Asaad hakuna atakayeshinda''.
Hatahivyo watu hao wawili walimjibu wakisema hawana muda wa kupoteza naye ila tu anawafurahisha.
Na baadaye bibi huyo anaonekana akiwaita 'punda',na watu hao wanaonekana wakicheka.
Kanda
hiyo ya Video iliwekwa katika mtandao wa facebook na Bint Jbeil,raia wa
kusini mwa Lebanon mwenye mtandao ulio maarufu kwa watu wa madhehebu ya
kishia.
Mtandao ulidai kwamba ni mama mzee aliyekuwa akiwakosoa wapiganaji wa IS(BBC)
إرسال تعليق