STAA wa zamani wa England aliyewahi kutamba na Machester United
kisha na Real Madrid, David Beckham amekiri kwamba mwanaye anayetabiriwa
kufuata nyayo zake, Brooklyn, hana hamu na kampani yake.
Beckham ametoa siri hiyo katika kipindi kimoja cha
televesheni alipokuwa akijibu swali juu ya nini familia yake
imemwandalia Brooklyn katika sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake
itakayofayika mwezi ujao.
“Nadhani sasa anataka uhuru wa kuwa na marafiki
zake, nadhani atakuwa na mlo wa jioni tofauti na ule wa familia. Kwa
sasa yupo katika umri unaonyesha hahitaji sana niwe karibu naye, hapendi
hata ninavyompeleka shuleni asubuhi, jambo siwezi kuliacha,” alisema.
Beckham (39), alisema bado anaamini kuwa ni wajibu
wake kuwa karibu na Brooklyn ijapokuwa mwanaye huyo anaonyesha
kutoendelea kufurahishwa na jambo hilo.
Kuhusu kutotakiwa kumpeleka shuleni, alisema:
“Sijafurahishwa naye katika hilo kwa sababu nimekuwa nikiamka saa moja
asubuhi ili kumpeleka darasani, ninapomwacha getini huwa namtakia masomo
na siku njema.”
إرسال تعليق