Ugonjwa wa Mama Diamond ni siri

SIKU chache baada ya mama wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Sanura Kassim kuripotiwa kuwa amelazwa nchini India kwa ajili ya matibabu, meneja wa mwanamuziki huyo amesema hiyo itaendelea kuwa siri ya familia.
Akizungumza na Mwanaspoti meneja huyo Hamis Taletale maarufu Babu Tale alisema hiyo ni siri ya familia na hawawezi kutoa majibu kuhusu lolote linaloendelea.
“Unataka kujua hali ya mgonjwa kwani wewe ndiye unatoa dawa, hili ni suala la kifamilia na hatuwezi kulitangaza magazetini,” alijibu babu Tale kwa kejeli.
Mama wa mwanamuziki huyo alipelekwa nchini India wiki mbili zilizopita kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua ghafla

Post a Comment

أحدث أقدم