Kama
kuna mtu ambaye Arsenal hawatamsahau katika mechi ya watani wa jadi wa
London dhidi yao na Tottenham, basi mtu huyu si mwingine zaidi ya
mshambuliaji chipukizi Harry Kane.
Mshambuliaji
huyo asiyeshikika, akatupia mabao mawili wavuni yaliyowapa ushindi wa
2-1 kwa Arsenal na kuzoa pointi tatu muhimu kwenye Ligi Kuu ya England
kupitia mchezo huo uliochezwa White Hart Lane.
Arsenal walikuwa kwa kwanza kufunga kwa goli la Mesut Ozil dakika ya 11, bao lililodumu hadi mapumziko.
Wakicheza
kwa kujiamini, Tottenham wakasawazisha katika dakika ya 58 pale Kane
alipounganisha mpira uliokolewa na kipa wa Arsenal David Ospina.

Dakika ya 86, Kane akaunganisha kwa kichwa krosi ya Bentaleb na kumwacha Ospina akiwa hana la kufanya. Likawa goli la pili.

Tottenham
(4-2-3-1): Lloris 6.5, Walker 7, Dier 7, Vertonghen 7.5, Rose 6.5,
Bentaleb 8, Mason 7.5 (Paulinho 95), Lamela 6.5 (Stambouli 90), Dembele
6.5 (Chadli 75), Eriksen 6.5, Kane 9

إرسال تعليق