
Chelsea
imeifunga Aston Villa 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu huku Manchester
City ikilazimisha sare ya 1-1 kwa Hull City na kufanya vijana wa Jose
Mourinho waongoze ligi kwa pointi saba safi.
Hazard
aliifungia Chelsea bao la kuongoza dakika ya 8 huku Okore
akiisawazishia Aston Villa dakika ya 48, likiwa ni bao la kwanza la
Premier League katika jumla ya masaa 11 waliyotumia katika mechi zao
kadhaa zilizopita.
Dakika ya 66 Chelsea wakafunga goli la ushindi kupitia kwa beki wake Ivanovic.


Mshambuliaji
mpya wa Chelsea Cuadrado alipata muda wa dakika 10 tu uwanjani pale
alipoingia dakika ya 80 kuchukua nafasi ya Willian.

Mchezaji
aliyetokea benchi James Milner ndiye aliyeikoa Manchester City dhid ya
Hull City kwa kuifungia bao la kusawazisha katika dakika za lala salama
akifuta bao la dakika ya 38 la David Meyler.

Southampton imecharuka kwa kuifunga Queens Park Rangers 1-0 kwa bao la Sadio Mane lililotinga wavuni dakika ya 90.
Matokeo ya mechi zote za Ligi Kuu zilizochezwa Jumamosi (ukiondoa wa Liverpool na Everton) ni kama ifuatavyo.
FT Tottenham Hotspur 2 - 1 Arsenal
FT Aston Villa 1 - 2 Chelsea
FT Leicester City 0 - 1 Crystal Palace
FT Manchester City 1 - 1 Hull City
FT Queens Park Rangers 0 - 1 Southampton
FT Swansea City 1 - 1 Sunderland
إرسال تعليق