Dar es Salaam. Madaktari katika Chuo cha Tiba
cha Amrita, Kochi huko India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa aina yake
wa kupandikiza mikono mipya kwa binadamu aliyekatika viungo hivyo.
Upandikizaji huo uliofanyika Januari 12 na 13,
ulifanikiwa kwa mara ya kwanza, baada mwanamume mwenye umri wa miaka 30,
aliyekatika mikono katika ajali ya treni kuwekewa mingine. Mikono hiyo
mipya ilichukuliwa kutoka kwa kijana wa miaka 24 aliyepata aliyefariki
katika ajali ya gari.
Mkuu wa kitengo cha upasuaji katika chuo hicho,
Profesa Subramania Iyer alisema: “Siku 14 baada ya upasuaji, mikono
ilikubaliwa na mwili na ikaanza kujongea, yaani aliyepandikizwa aliweza
kuisogeza huku na kule. Mgonjwa alitolewa chumba cha wagonjwa mahututi
na huduma nyingine za kumchunguza ziliendelea.”
Daktari katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya
Fahamu Hospitali ya Muhimbili (Moi), Profesa John Kahamba alisema hiyo
si mara ya kwanza kwa upandikizaji wa mikono kufanyika duniani kwani na
tofauti kubwa na upandikizaji wa figo au ini.
Jinsi unavyofanyika
Profesa Kahamba alisema upasuaji huo unafanyika
kwa kuhakiki mambo mbalimbali ikiwamo uwiano wa kundi la damu, uhai wa
seli na misuli na mishipa midogo ya fahamu.
“Upasuaji mkubwa hufanyika, pamoja na kuangalia
uwiano wa damu lakini lazima jopo la madaktari wenye kazi tofauti
lifanye kazi kwa pamoja. Kwa mfano, wanaounganisha misuli na mishipa
midogomidogo na hata wale wa kuhakiki uhai wa seli,” alisema.
Profesa Kahamba alisema kama upandikizaji wa figo unavyofanyika, kadhalika upandikizaji wa mikono unahitaji umakini wa muda.
Anasema iwapo utachelewa kuunganisha mikono baada
ya kuitoa, seli zake zinaweza kufa na kushindwa kufanya kazi
zitakapopandikizwa kwenye mwili.
“Katika hili, dawa za kuufanya mwili kukubali
mikono hiyo lazima zipatikane kwa sababu mwili una tabia ya kukataa vitu
vigeni,” alisema.
Profesa Kahamba alisema upandikizaji wa aina hii
ni mkubwa na unahitaji ushirikiano wa kada kadhaa za wataalamu wa afya
na vitendea kazi sahihi na vya kisasa.
Post a Comment