Hotuba ya Mwenyekiti wa CCM inaweza kuwa ni hofu ya uchaguzi Mkuu

Februari Mosi, CCM ilisherehekea miaka 38 tangu kaunzishwa kwake.
Hiki ni kipindi kirefu na kama ni umri wa mtu, huyu si mtoto tena, bali ni mtu mzima anayepaswa kuwajibika katika maisha yake na maisha ya wenzake katika jamii anamoishi.
Siku hii ya kuzaliwa CCM kwa kawaida hufanyika Februari 5. Kwa mwaka huu ingeangukia siku ya Alhamisi, lakini cha kushangaza ilirudishwa nyuma na kuadhimishwa siku ya Bwana, yaani Jumapili kwa sababu ambazo hazijulikani, lakini inaruhusiwa.
Mimi binafsi nilibahatika kuwa katika mji wa Songea mkoani Ruvuma, kulikofanyika sherehe hizo. Mkoa huo ndiko kwangu kiasili.
Ni heshima kubwa kupewa nafasi ya kuandaa sherehe ya kitaifa kwani ni nafasi nyeti na kila mkoa unaitafuta. Bado haikufahamika kigezo kilichotumiwa kupeleka sherehe hizi mkoani Ruvuma ambako maendeleo bado yako nyuma katika nyanja mbalimbali.
Idadi ya watu waliojaa kwenye Uwanja wa Majimaji haikuwa ndogo, lakini kwa upande mmoja ukipita mitaani uliweza kuona watu wengi wakiendelea na shughuli zao.
Nilipojaribu kuwadodosa baadhi ya wananchi wa mji wa Songea, inakuwaje uwanja umefurika lakini bado wengine wanaonekana barabarani? jibu nililopewa ni kwamba “watu waliofurika ndani ya uwanja waliletwa na malori na mabasi kutoka katika kila kata ndani ya mkoa huo”.
“Padri Mapunda, hawa watu waliofurika Uwanja wa Majimaji si Wanasongea, bali wengi wao wametoka mkoa mzima na hata Kanda ya Nyanda za Juu Kusini. Ndani ya mkoa kila kata waliletwa watu 10 na pia shule zote za shule ya msingi na sekondari hapa mjini waliamrishwa wahudhurie na sharti wafike bila sare,” alisema mwananchi mmoja.
Hofu ya Uchaguzi Mkuu
Leo hoja yangu si watu waliofurika nikijua kwamba Ruvuma haina matukio mengi ya kitaifa kama hayo. Kwa hiyo watu wengi wangelipenda kuhudhuria kwenye tukio kama hilo. Mimi hoja yangu kubwa leo ni hotuba iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete. Kwa upande wangu hotuba ile ilikuwa imejaa hofu ya Uchaguzi Mkuu.
Oktoba mwaka huu, Watanzania tutapata tena fursa ya kumchagua Rais wa awamu ya tano ambaye atakuwa mrithi wa Rais wetu wa sasa.
Ni wazi huu ni uchaguzi wa kihistoria; kwanza kwa sababu unatanguliwa na Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa ambayo mimi naiita “Katiba ya CCM”. Ni Katiba iliyotupilia mbali maoni ya wananchi yaliyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba na wakapachika maoni ya chama
- Mwananchi

Post a Comment

Previous Post Next Post