Februari Mosi, CCM ilisherehekea miaka 38 tangu kaunzishwa kwake.
Hiki ni kipindi kirefu na kama ni umri wa mtu,
huyu si mtoto tena, bali ni mtu mzima anayepaswa kuwajibika katika
maisha yake na maisha ya wenzake katika jamii anamoishi.
Siku hii ya kuzaliwa CCM kwa kawaida hufanyika
Februari 5. Kwa mwaka huu ingeangukia siku ya Alhamisi, lakini cha
kushangaza ilirudishwa nyuma na kuadhimishwa siku ya Bwana, yaani
Jumapili kwa sababu ambazo hazijulikani, lakini inaruhusiwa.
Mimi binafsi nilibahatika kuwa katika mji wa Songea mkoani Ruvuma, kulikofanyika sherehe hizo. Mkoa huo ndiko kwangu kiasili.
Ni heshima kubwa kupewa nafasi ya kuandaa sherehe
ya kitaifa kwani ni nafasi nyeti na kila mkoa unaitafuta. Bado
haikufahamika kigezo kilichotumiwa kupeleka sherehe hizi mkoani Ruvuma
ambako maendeleo bado yako nyuma katika nyanja mbalimbali.
Idadi ya watu waliojaa kwenye Uwanja wa Majimaji
haikuwa ndogo, lakini kwa upande mmoja ukipita mitaani uliweza kuona
watu wengi wakiendelea na shughuli zao.
Nilipojaribu kuwadodosa baadhi ya wananchi wa mji
wa Songea, inakuwaje uwanja umefurika lakini bado wengine wanaonekana
barabarani? jibu nililopewa ni kwamba “watu waliofurika ndani ya uwanja
waliletwa na malori na mabasi kutoka katika kila kata ndani ya mkoa
huo”.
“Padri Mapunda, hawa watu waliofurika Uwanja wa
Majimaji si Wanasongea, bali wengi wao wametoka mkoa mzima na hata Kanda
ya Nyanda za Juu Kusini. Ndani ya mkoa kila kata waliletwa watu 10 na
pia shule zote za shule ya msingi na sekondari hapa mjini waliamrishwa
wahudhurie na sharti wafike bila sare,” alisema mwananchi mmoja.
Hofu ya Uchaguzi Mkuu
Leo hoja yangu si watu waliofurika nikijua kwamba
Ruvuma haina matukio mengi ya kitaifa kama hayo. Kwa hiyo watu wengi
wangelipenda kuhudhuria kwenye tukio kama hilo. Mimi hoja yangu kubwa
leo ni hotuba iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete. Kwa upande wangu
hotuba ile ilikuwa imejaa hofu ya Uchaguzi Mkuu.
Oktoba mwaka huu, Watanzania tutapata tena fursa ya kumchagua Rais wa awamu ya tano ambaye atakuwa mrithi wa Rais wetu wa sasa.
Ni wazi huu ni uchaguzi wa kihistoria; kwanza kwa
sababu unatanguliwa na Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa ambayo
mimi naiita “Katiba ya CCM”. Ni Katiba iliyotupilia mbali maoni ya
wananchi yaliyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba na wakapachika
maoni ya chama
- Mwananchi
إرسال تعليق