MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe, amemwambia
kocha wa timu hiyo, Hans van Der Pluijm kuwa, anataka kucheza na Mrisho
Ngassa.Ngassa alianza na Tambwe kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho
Afrika dhidi ya BDF na Mrundi huyo akafanikiwa kupachika mabao mawili.
Mrundi huyo, akiwa anaichezea Simba, aliwahi kutamka kuwa anatamani
siku moja kucheza na viungo washambuliaji wa Yanga, Ngassa na Simon
Msuva, kutokana na uwezo wao wa kupiga krosi safi kwa
washambuliaji.Katika mchezo huo, Tambwe alifunga mabao yake kwa mipira
kutoka kwa Ngassa na Haruna Niyonzima.
Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema katika mechi dhidi
ya BDF XI FC ya Botswana, kiungo huyo alimng’arisha kwa kumpigia mipira
mingi ya krosi na kufanikiwa kufunga mabao mawili.
“Yanga wapo wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza soka watakaoanza kwenye kikosi cha kwanza kiukweli, lakini Ngassa yeye uzuri wake anajua kutengeneza mabao kwa kupiga krosi na pasi safi za kufunga mabao.
“Yanga wapo wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza soka watakaoanza kwenye kikosi cha kwanza kiukweli, lakini Ngassa yeye uzuri wake anajua kutengeneza mabao kwa kupiga krosi na pasi safi za kufunga mabao.
“Ninaamini kama kocha akiendelea kunipanga naye katika kikosi cha
kwanza, basi nitafunga sana mabao kwa sababu tayari tumezoeana na
kuendana aina ya uchezaji ndani ya uwanja na ninapenda ushirikiano wake.
“Ngassa anajua aina ipi ya mipira ya krosi na pasi ninazozitaka ndani
ya uwanja, hiyo ni baada ya kocha kutuchezesha mara kwa mara mazoezini
na kutupa mbinu mbalimbali za kufunga, namuomba aendelee kutuamini,”
alisema Tambwe ambaye msimu uliopita alichukua ufungaji bora akifunga 19
katika ligi kuu akiwa na kikosi cha Simba
إرسال تعليق