Tambwe amlilia Ngassa

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe, amemwambia kocha wa timu hiyo, Hans van Der Pluijm kuwa, anataka kucheza na Mrisho Ngassa.Ngassa alianza na Tambwe kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF na Mrundi huyo akafanikiwa kupachika mabao mawili.
Mrundi huyo, akiwa anaichezea Simba, aliwahi kutamka kuwa anatamani siku moja kucheza na viungo washambuliaji wa Yanga, Ngassa na Simon Msuva, kutokana na uwezo wao wa kupiga krosi safi kwa washambuliaji.Katika mchezo huo, Tambwe alifunga mabao yake kwa mipira kutoka kwa Ngassa na Haruna Niyonzima.
Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema katika mechi dhidi ya BDF XI FC ya Botswana, kiungo huyo alimng’arisha kwa kumpigia mipira mingi ya krosi na kufanikiwa kufunga mabao mawili.
 “Yanga wapo wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza soka watakaoanza kwenye kikosi cha kwanza kiukweli, lakini Ngassa yeye uzuri wake anajua kutengeneza mabao kwa kupiga krosi na pasi safi za kufunga mabao.
“Ninaamini kama kocha akiendelea kunipanga naye katika kikosi cha kwanza, basi nitafunga sana mabao kwa sababu tayari tumezoeana na kuendana aina ya uchezaji ndani ya uwanja na ninapenda ushirikiano wake.
“Ngassa anajua aina ipi ya mipira ya krosi na pasi ninazozitaka ndani ya uwanja, hiyo ni baada ya kocha kutuchezesha mara kwa mara mazoezini na kutupa mbinu mbalimbali za kufunga, namuomba aendelee kutuamini,” alisema Tambwe ambaye msimu uliopita alichukua ufungaji bora akifunga 19 katika ligi kuu akiwa na kikosi cha Simba

Post a Comment

Previous Post Next Post