Majibu ya Ommy Dimpoz kuhusiana na picha zilizoenea akiwa na Ex wa Diamond Platnumz

.
Miongoni mwa stori zilizochukua headline mitandaoni hata kwenye magazeti ni kuhusu picha ya hitmaker wa ‘Ndangushima’ Ommy Dimpoz akiwa na ex wa Diamond Platnumz ,Wema Sepetu kitandani wamelala pamoja na picha zingine zilizozua mjadala mkubwa.
Sasa leo Feb 12 Ommy Dimpoz ame amplify kwenye Amplifaya ya Clouds FM na  kusema ;Ni picha tu mimi naona kama ni picha zingine tu za kawaida,  sasa nimeshindwa kuelewa kwanini labda zimetengeneza sana stori  kwasababu mimi naona sio mara yangu kwanza kupiga picha na Wema hata uki google utaona tunapicha nyingi sana kwa hiyo sijaelewa kwanini zimeleta stori
May be nafikikiri zilizotengeneza stori zaidi ni hizi ambazo zinaonesha tuko chumbani kwasababu mimi nilikuwa nimelala kiukweli  na tulikuwa tunakaa kwenye apartment moja nilikua nimeshtukia picha zipo kwenye mitandao unajua unavyokaa kwenye apartment kwasababu tulienda kwenye matembezi binafsi na washikaji wengine tulikua wengi wengi kidogo tulienda South Africa unajua mnavyokaa kama familia kunakuwa na mambo ya utani utani nimeshtukia tu picha zimeenea kwahiyo hata watu wakiniuliza ninawambia wamuuliza aliyepiga picha hizo
Millardayo ; “…Wengi wanafahamu kuwa wewe ni mshikaji wa Diamond Platnumz imekuaje sasa hivi kuonekana kwenye picha na Ex wa Diamond Platnumz,Wema Sepetu…?”
Ommy Dimpoz ; “…Sidhani kama kuna tatizo kwasababu hawa wote ni watu wangu nimefahamia nao siku nyingi nimekuwa nao karibu katika kipindi tofauti kabla hawajakuwa kwenye uhusiano mimi tayari ni watu wangu sidhani mimi nianze kuelezea sijui ooh nilikuwa labda na Wema sehemu, Wema ni mshikaji wangu tangia  siku nyingi kwa hiyo  hata kama alikuwa katika  uhusiano na Diamond yakatokea mahusiano yao pengine hayapo sasa  hivi hayawezi kunifanya mimi kuharibu ushikaji wangu kwasababu hivyo ni vitu vyao  personal…“Alisema.

Post a Comment

أحدث أقدم