PENNY: NIMEPATA MCHUMBA MUNGU NI MWEMA

Mtangazaji aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul, ‘Diamond’,  Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameibuka na kusema kuwa anashukuru amepata mchumba ila suala la ndoa siyo la leo wala kesho.


Mtangazaji aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul, ‘Diamond’,  Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Akipiga stori na juzikati, Penny alisema wengi wamekuwa wakitaka kusikia suala la yeye kuolewa baada ya kubainika ana mchumba lakini mwenyewe anasema hajafikiria hilo la kuitwa mke kwa sasa.

“Kwenye hilo la kufunga ndoa naweza kusema bado niponipo sana, yapo mambo yangu ambayo lazima niyakamilishe kabla ya kuolewa, ndoa si mchezo, kujipanga ni muhimu,” alisema Penny.

Post a Comment

أحدث أقدم